Jawabu: Ni kumpenda Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Amesema Allah Mtukufu: "Na wale walioamini wanamapenzi makubwa kwa Mwenyezi Mungu" [Suratul Baqara: 165].
Kumpenda mtume - rehema na amani ziwe juu yake
Amesema: "Namuapia yule ambaye nafsi yangu ipo mikononi mwake, hawezi kuwa na imani mmoja wenu mpaka nipendeke kwake zaidi kuliko mtoto wake na mzazi wake". Imepokelewa na Al-Bukhaariy
Kuwapenda waumini, na kuwapendelea kheri kwao kama unavyoipendelea nafsi yako.
Amesema Mtume Sala na salamu ziwe juu yake: "Hawezi kuwa na imani mmoja wenu mpaka ampendelee ndugu yake anachokipenda yeye katika nafsi yake" Imepokelewa na Al-Bukhaariy