Jawabu: -Kuwahurumia wazee na kuwaheshimu.
- Kuwahurumia wadogo na watoto.
- Kumhurumia masikini na mwenye shida.
-Kuwahurumia wanyama kwa kuwalisha na kutowaudhi.
Na katika hili ni kauli ya Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake: "Mfano wa waumini katika kupendana kwao na kuhurumiana kwao na kufanyiana kwao upole, ni kama mfano wa kiwiliwili, kinapopata tabu kiungo kimoja vinaitana kwa ajili ya hicho kimoja viungo vyote kwa kukesha na maumivu" Wamekubaliana Bukhari na Muslim. Na Amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu rehema na Amani ziwe juu yake. "Wenye huruma huwahurumia Ar-Rahmani -Mwingi wa huruma-, wahurumieni watu wa ardhini atakuhurumieni aliyeko mbinguni." Imepokelewa na Abudaud na Tirmidhiy.