Jawabu: Ni watu kusaidizana wao kwa wao katika haki na mambo ya kheri.
Namna za kusaidizana:
* Kusaidizana katika kurudisha haki za watu.
* Kusaidizana katika kumzuia mwenye kudhulumu.
* Kusaidizana katika kukidhi mahitaji ya watu na masikini.
* Kusaidina katika kila kheri.
* Kutosaidizana katika madhambi na maudhi na uadui.
Amesema Allah Mtukufu: "Na saidianeni katika wema na uchamungu na wala msisaidiane katika madhambi na kufanya uovu,na muogopeni Mwenyezi Mungu kwa hakika Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu" [Suratul Maidah: 2] Amesema Mtume Sala na salamu ziwe juu yake: "Muumini kwa muumini mwenzake ni kama jengo moja; linajiimarisha baadhi yake kwa baadhi" Wamekubaliana Bukhari na Muslim. Amesema Mtume Sala na salamu ziwe juu yake: "Muislamu ndugu yake ni muislamu, asimdhulumu na wala asimsaliti, na atakayekuwa katika shida ya ndugu yake, basi Mwenyezi Mungu naye atakuwa katika shida yake, na atakayetatua kwa muislamu matatizo, basi na Mwenyezi Mungu atamtatulia tatizo katika matatizo ya siku ya kiyama, na atakayemsitiri muislamu, Mwenyezi Mungu naye atamsitiri siku ya kiyama". Wamekubaliana Bukhari na Muslim.