Jawabu: Ni kutokuvumilia juu ya kumtii Mwenyezi Mungu, kutosubiri katika kuyaendea maasi, kulalamika na kuchukia makadirio kwa kuzungumza au vitendo vinavyoonyesha kutoridhishwa na makadirio.
Katika namna zake:
Kutamani kifo.
Kupiga mashavu.
Kuchana nguo.
Kusambaza nywele, kwa itikadi za kutoridhishwa na msiba uliotokea.
Kujiombea maangamivu.
Amesema Mtume Sala na salamu ziwe juu yake: "Hakika ukubwa wa malipo huendana sawa pamoja na ukubwa wa matatizo, na hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu anapowapenda watu huwapa mtihani; atakayeridhia atapata radhi, na atakayechukia atapata hasira (za Mwenyezi Mungu)." Kaipokea Tirmidhi na bin Majah