Jawabu: Kusubiri juu ya kumtii Mwenyezi Mungu Mtukufu.
- Kusubiri kutoyaendea maasi.
-kusubiri juu ya makadirio ya Mwenyezi Mungu yaumizayo, na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kila hali.
Amesema Allah Mtukufu: "Na Mwenyezi Mungu anawapenda wenye kusubiri" [Surat Al Imrani: 146] Amesema Mtume Sala na salamu ziwe juu yake: "Ajabu iliyoje ya jambo la muumini, hakika jambo lake lote ni kheri, na hakuna hilo kwa yeyote ila kwa muumini: akipatwa na jambo lenye kufurahisha anashukuru ikawa hilo ni kheri kwake, na akipatwa na madhara anasubiri likawa hilo ni kheri kwake." Imepokelewa na Imamu Muslim