Jawabu: 1- Ninapohisi maumivu; ninaweka mkono wangu wa kulia sehemu inayouma, na ninasema: "Bismillaah" Mara tatu, na ninasema: "Audhu bi izzatillaahi waquduratihi min sharri maa ajidu wa uhaadhir" Mara saba, yaani: Ninajilinda kwa utukufu wa Mwenyezi Mungu na uwezo wake kutokana na shari za yale ninayoyapata na ninachukua hadhari.
2- Ninaridhika na yale aliyoyakadiria na Mwenyezi Mungu na ninasubiri.
3- Ninafanya haraka kumtembelea ndugu yangu akiwa mgonjwa, na ninamuombea dua, na wala sikai kwake muda mrefu.
4- Ninamfanyia kisomo bila ya yeye kuniomba.
5- Ninamuhusia kuvumilia, kuomba dua, kuswali, na kuwa twahara kwa kadiri awezavyo.
6- Dua ya mgonjwa: "As alullaahal Adhwiim Rabbal Arshil Adhwiim an yash-fiyaka" Mara saba, Yaani: Namuomba Allah Mtukufu, Mola wa Arshi Tukufu akuponye.