Swali: 24- Eleza adabu za kupiga chafya.

Jawabu: 1- Kuweka mkono au nguo au kitambaa wakati wa kupiga chafya.

2- Kumshukuru Mwenyezi Mungu baada ya kupiga chafya kwa kusema: "Alhamdulilllah"

3- Na aliyemsikia aseme kumwambia ndugu yake: "Yar-hamukallaah" Mwenyezi Mungu akuhurumie.

Akisema kumwambia hivyo: Basi naye aseme: "Yah-diikumullaahu wayuslih baalakum" Akuongozeni Mwenyezi Mungu na akutengenezeeni mambo yenu".