Swali: 9- Soma Suratu Quraishi na uitafsiri.

Jawabu: Suratu Quraishi na tafsiri yake:

Naanza kusoma Qur’an kwa jina la Mwenyezi Mungu nikiomba msaada Wake. «Allah» ni jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa baraka Mwenye kutukuka, Anayestahiki kuabudiwa na sio mwingine. Nalo ni jina mahsusi zaidi miongoni mwa majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, na haitwi kwa jina hili yeyote isipokuwa Yeye Aliyetakasika na sifa za upungufu. «Al-Raḥmān» Mwenye rehema nyingi Ambaye rehema Zake zimewanea viumbe vyote. «Al-Raḥīm» mwenye kuwarehemu Waumini. Na majina mawili haya, kati ya majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, yanakusanya uthibitishaji wa sifa ya urehemefu kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kama unavyonasibiana na haiba Yake.

(Kwa ajili ya kuzoea Makuraishi) (1) (Kuzoea kwao misafara ya kusi na kaskazi) (2) "Basi, wamshukuru na kumuabudu Bwana wa Nyumba hii ya Alkaaba, Ambaye kwa ajili Yake wametukuzwa, na wampwekeshe na kumtakasia ibada." "Ambaye Amewapa wao chakula wakati wa njaa kali na akawapa amani na utulivu kutokana na hofu kubwa na mbabaiko." [Suratu Quraishi: 1-4]

Tafsiri:

(Kwa ajili ya kuzoea Makuraishi) (1) Makusudio ya hilo na kile walichokuwa wamekizoea miongoni mwa safari za masika na kiangazi.

(Kuzoea kwao misafara ya kusi na kaskazi) (2) Safari ya masika walikuwa wakienda Yemen, na safari ya kiangazi walikuwa wakienda Sham (Siria, iraq, Jordan, Palestina) wakiwa na amani.

"Basi, wamshukuru na kumuabudu Bwana wa Nyumba hii ya Alkaaba, Ambaye kwa ajili Yake wametukuzwa, na wampwekeshe na kumtakasia ibada." Basi na wamuabudu Mwenyezi Mungu Mola wa nyumba hii peke yake, aliyewafanyia wepesi safari hizi, na wala wasimshirikisha na yeyote.

"Ambaye Amewapa wao chakula wakati wa njaa kali na akawapa amani na utulivu kutokana na hofu kubwa na mbabaiko." Aliyewalisha wakati wa njaa, na akawapa amani na kuwaondolea hofu, kwa kile alicho kiweka katika nyoyo za waarabu kwa sababu ya utukufu wa msikiti mtukufu, basi walikuwa wakiwatukuza wakazi wa maeneo ya msikiti huo mtukufu.