Swali: 8- Soma suratul Fil na uitafsiri.

Jawabu: Suratul Fil na tafsiri yake:

Naanza kusoma Qur’an kwa jina la Mwenyezi Mungu nikiomba msaada Wake. «Allah» ni jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa baraka Mwenye kutukuka, Anayestahiki kuabudiwa na sio mwingine. Nalo ni jina mahsusi zaidi miongoni mwa majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, na haitwi kwa jina hili yeyote isipokuwa Yeye Aliyetakasika na sifa za upungufu. «Al-Raḥmān» Mwenye rehema nyingi Ambaye rehema Zake zimewanea viumbe vyote. «Al-Raḥīm» mwenye kuwarehemu Waumini. Na majina mawili haya, kati ya majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, yanakusanya uthibitishaji wa sifa ya urehemefu kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kama unavyonasibiana na haiba Yake.

"Je hujui, ewe Mtume, namna Alivyowafanya Mola wako watu wa ndovu: Abraha Mhebeshi na jeshi lake ambalo alikuja nalo ili kuivunja Alkaba tukufu?" "Kwani Hakuijaalia mipango yao mibaya waliyoifanya ni yenye kuvunjika na kupita patupu?" "Na Aliwapelekea makundi yaliyofuatana, ya ndege waliokuwa wakiwatupia wao vijiwe vya udongo mkavu mgumu." Akawapondaponda, wakawa ni kama majani makavu yaliyoliwa na wanyama na halafu kutupwa." [Suratul Fil: 1-5.]

Tafsiri:

"Je hujui, ewe Mtume, namna Alivyowafanya Mola wako watu wa ndovu: Abraha Mhebeshi na jeshi lake ambalo alikuja nalo ili kuivunja Alkaba tukufu?" Hivi hujui ewe Mtume ni jinsi gani alimfanya Mola wako Abraha na watu wa ndovu walipotaka kuibomoa Alkaaba?!

"Kwani Hakuijaalia mipango yao mibaya waliyoifanya ni yenye kuvunjika na kupita patupu?" Aliifanya Mwenyezi Mungu mipango yao mibaya ya kuibomoa kuwa ni hasara, hawakufanikisha walilotamani la kuwaondoa watu katika Alkaaba, na wala hawakufanikisha chochote.

"Na Aliwapelekea makundi yaliyofuatana," Na akawatumia ndege, waliowajia makundi kwa makundi.

ya ndege waliokuwa wakiwatupia wao vijiwe vya udongo mkavu mgumu." Waliwapiga kwa mawe ya udongo mgumu.

Akawapondaponda, wakawa ni kama majani makavu yaliyoliwa na wanyama na halafu kutupwa." Mwenyezi Mungu akawafanya kama majani ya mimea yaliyotafunwa na mnyama na akayakanyaga.