Jawabu: Suratul Asri na tafsiri yake:
Naanza kusoma Qur’an kwa jina la Mwenyezi Mungu nikiomba msaada Wake. «Allah» ni jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa baraka Mwenye kutukuka, Anayestahiki kuabudiwa na sio mwingine. Nalo ni jina mahsusi zaidi miongoni mwa majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, na haitwi kwa jina hili yeyote isipokuwa Yeye Aliyetakasika na sifa za upungufu. «Al-Raḥmān» Mwenye rehema nyingi Ambaye rehema Zake zimewanea viumbe vyote. «Al-Raḥīm» mwenye kuwarehemu Waumini. Na majina mawili haya, kati ya majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, yanakusanya uthibitishaji wa sifa ya urehemefu kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kama unavyonasibiana na haiba Yake.
"Na apa kwa wakati wa laasiri" "Hakika wanadamu wako kwenye maangamivu na upungufu". "Isipokuwa wale waliomuamini Mwenyezi Mungu, wakafanya matendo mema, wakausiana wao kwa wao kushikamana na haki, kufanya matendo ya kumtii Mwenyezi Mungu na kusubiri juu yake" [1]. [Suratul Asri: 1-3]
Tafsiri:
"Na apa kwa wakati wa laasiri": Ameapa Mtukufu kwa nyakati.
"kwamba wanadamu wako kwenye maangamivu na upungufu". Yaani: Kila mwanadamu yuko katika mapungufu na maangamivu.
"Isipokuwa wale waliomuamini Mwenyezi Mungu, wakafanya amali njema, wakausiana wao kwa wao kushikamana na haki, kufanya matendo ya kumtii Mwenyezi Mungu na kusubiri juu yake" Isipokuwa yule atakayeamini na akafanya matendo mema, na pamoja na hilo walingania katika haki na wakasubiri juu ya hilo, hawa ndio waliookoka na hasara.