Swali: 5- Soma Suratut Takaathur na uitafsiri.

Jawabu: Suratut Takaathur na tafsiri yake:

Naanza kusoma Qur’an kwa jina la Mwenyezi Mungu nikiomba msaada Wake. «Allah» ni jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa baraka Mwenye kutukuka, Anayestahiki kuabudiwa na sio mwingine. Nalo ni jina mahsusi zaidi miongoni mwa majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, na haitwi kwa jina hili yeyote isipokuwa Yeye Aliyetakasika na sifa za upungufu. «Al-Raḥmān» Mwenye rehema nyingi Ambaye rehema Zake zimewanea viumbe vyote. «Al-Raḥīm» mwenye kuwarehemu Waumini. Na majina mawili haya, kati ya majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, yanakusanya uthibitishaji wa sifa ya urehemefu kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kama unavyonasibiana na haiba Yake.

"Kumekushughulisheni kutaka wingi" "Kujishughulisha kwenu na hilo kumeendelea mpaka mkawa makaburini na mkazikwa humo." "Siyo namna hii kunatakiwa kuwapumbaze kushindana kwa wingi wa mali. Itawadhihirikia kuwa Nyumba ya Akhera ni bora kwenu." "Kisha tahadharini mtajua mwisho mbaya wa kutojishughulisha na Akhera." "Siyo namna hii inatakiwa iwashughulishe kushindana kwa wingi wa mali. Lau mnajua ukweli, mngalirudi nyuma na mngalishughulika na kuokoa nafsi zenu kutoka kwenye maangamivu." "Hakika bila shaka mtauona moto wa Jahanam" "Kisha mtauona bila shaka!" "Kisha mtaulizwa kuhusu kila aina ya starehe mliyokuwa nayo." [Suratut Takaathur: 1-8]

Tafsiri:

"kumekushughulisheni kutaka wingi": Kumekushughulisheni enyi watu kujifaharisha kwa mali na watoto mkaacha kumtii Mwenyezi Mungu.

"Mkaendelea kujishughulisha kwenu mpaka mkaingia makaburini" Yaani: Mpaka mkafa mkaingia makaburini mwenu.

"Si hivyo, mtakuja jua" Hamkutakiwa kuwashughulishe huko kujifaharisha kwa hayo mkaacha kumtii Mwenyezi Mungu, mtakuja kujua mwisho wa huko kujishughulisha.

"Kisha, si hivyo, mtakuja jua": Mtakuja jua mwisho wake.

"Si hivyo, lau mngelijua kikweli kweli": Yaani: Kiukweli laiti mngelijua kwa hakika kuwa nyinyi mtafufuliwa mbele ya Mwenyezi Mungu, nakuwa yeye atakulipeni juu ya matendo yenu, kwa kitendo chenu cha kujishughulisha na kujifaharisha kwa mali na watoto.

"Hakika bila shaka mtauona moto wa Jahim" Namuapa Mwenyezi Mungu mtaushuhudia moto siku ya kiyama.

"Kisha hakika mtauona bila shaka" Kisha mtaushuhudia kuushuhudia kwa uhakika kusikokuwa na shaka ndani yake.

"Kisha mtaulizwa kuhusu kila aina ya starehe mliyokuwa nayo." Kisha bila shaka atakuulizeni Mwenyezi Mungu katika siku hiyo juu ya yale aliyokuneemesheni miongoni mwa afya na utajiri na mengineyo.