Swali: 2- Soma Aadiyaat na uitafsiri.

Jawabu: Suratul Aaadiyaati na tafsiri yake:

Naanza kusoma Qur’an kwa jina la Mwenyezi Mungu nikiomba msaada Wake. «Allah» ni jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa baraka Mwenye kutukuka, Anayestahiki kuabudiwa na sio mwingine. Nalo ni jina mahsusi zaidi miongoni mwa majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, na haitwi kwa jina hili yeyote isipokuwa Yeye Aliyetakasika na sifa za upungufu. «Al-Raḥmān» Mwenye rehema nyingi Ambaye rehema Zake zimewanea viumbe vyote. «Al-Raḥīm» mwenye kuwarehemu Waumini. Na majina mawili haya, kati ya majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, yanakusanya uthibitishaji wa sifa ya urehemefu kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kama unavyonasibiana na haiba Yake.

"Mwenyezi Mungu Anaapa kwa farasi wenye kwenda mbio katika njia Yake kumkabili adui, huku wakitoa sauti kwa kasi ya kukimbia." "Wakitoa moto kwa kupiga kwato zao chini." "Wakishambulia wakati wa asubuhi". "Wakirusha vumbi kwa mbio zao." "Wakiwatia kati makundi ya maadui, kwa kuwazunguka kwa vipando vyao, "Hakika binadamu ni mkanushaji sana wa neema za Mola wake." "Na yeye anakubali ukanushaji wake." "Na yeye ana pupa sana ya mali." "Kwani binadamu hajui linalomngojea mbele yake, pindi Mwenyezi Mungu Atakapo watoa wafu makaburini waende kuhesabiwa na kulipwa?" "Na (kwani yeye hajui) kuwa yatatolewa yaliyomo ndani ya vifua: mema au maovu?" "Kwa hakika Mola wao Mlezi siku hiyo bila ya shaka atakuwa na khabari zao wote!" [Suratul Aadiyaat: 1-11]

Tafsiri:

"Mwenyezi Mungu Anaapa kwa farasi wenye kwenda mbio katika njia Yake kumkabili adui, wakitoa sauti kwa kasi ya kukimbia." Ameapa Mwenyezi Mungu kwa Farasi ambao wanakwenda mbio mpaka inasikika sauti ya pumzi zao kwa sababu ya kasi kubwa ya kukimbia.

"Wakitoa moto kwa kupiga kwato zao chini." Na ameapa pia kwa Farasi ambao wanawasha moto kwa kwato zao zinapogusa miamba kwa sababu ya kuikanyaga kwa nguvu.

"Wakishambulia wakati wa asubuhi" Na amewaapia Farasi ambao wanawashambulia maadui wakati wa asubuhi.

"Wakarusha vumbi kwa mbio zao." Yaani: Wakatimua vumbi kwa mbio zao.

"Wakiwatia kati,maadui kuwazunguka kwa vipando vyao, mkusanyiko wa maadui" Yaani: Wakalitia kati kwa Farasi zao kundi katika maadui.

"Hakika binadamu ni mkanushaji sana wa neema za Mola wake." Yaani: Hakika mwanadamu ni mchoyo katika mambo mazuri yale anayoyataka kutoka kwake Mola wake.

"Na yeye anakubali ukanushaji wake" Na hakika yeye juu ya kuzuia kwake mambo mazuri ni shahidi, hawezi kulipinga hilo kwa sababu liko wazi.

"Na yeye ana pupa sana ya mali." Yaani: Na hakika yeye ni mkosefu kwa kupenda kwake mali anayoifanyia ubahili.

"Kwani binadamu hajui linalomngojea mbele yake, pindi Mwenyezi Mungu Atakapowatoa wafu makaburini waende kuhesabiwa na kulipwa?" Hivi kwani hajui huyu mwanadamu anayedanganyika na uhai wa Dunia kuwa Mwenyezi Mungu atakapoyafufua makaburi katika wafu na akawatoa kutoka katika Ardhi kwa ajili ya hesabu na malipo kuwa jambo halitokuwa kama anavyodhania?!.

"Na (kwani yeye hajui) kuwa yatatolewa yaliyo ndani ya vifua: mema au maovu?" Na yakawekwa wazi na yakabainishwa yaliyoko ndani ya nyoyo miongoni mwa nia na itikadi na mengineyo.

"Hakika Mola wao kwao na kwa amali zao, Siku Hiyo, ni Mtambuzi; hakuna chenye kufichikana Kwake" Yaani: Hakika Mola wao katika hilo siku hiyo atakuwa na habari, hakuna chochote kitakachofichikana kwake katika matendo ya waja wake, na atawalipa kwayo.