Jawabu: Suratuz zalzala na tafsiri yake:
Naanza kusoma Qur’an kwa jina la Mwenyezi Mungu nikiomba msaada Wake. «Allah» ni jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa baraka Mwenye kutukuka, Anayestahiki kuabudiwa na sio mwingine. Nalo ni jina mahsusi zaidi miongoni mwa majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, na haitwi kwa jina hili yeyote isipokuwa Yeye Aliyetakasika na sifa za upungufu. «Al-Raḥmān» Mwenye rehema nyingi Ambaye rehema Zake zimewanea viumbe vyote. «Al-Raḥīm» mwenye kuwarehemu Waumini. Na majina mawili haya, kati ya majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, yanakusanya uthibitishaji wa sifa ya urehemefu kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kama unavyonasibiana na haiba Yake.
"Itakapotikiswa ardhi mtikiso wa nguvu." "Na ikatoa vilivyomo ndani yake: kama wafu" "Na akauliza binadamu, kwa babaiko, «leo ardhi ina nini?» "Siku ya Kiyama ardhi itatoa habari ya mambo yaliyofanywa juu yake mazuri na mabaya." "kwa kuwa Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na kutukuka, Ameiamuru itoe habari ya mambo iliyofanyiwa." "Siku hiyo wataondoka kutoka kwenye kisimamo cha Hesabu wakiwa makundi, ili Mwenyezi Mungu Awaonyeshe waliyoyatenda, mazuri na mabaya, na Awalipe kwayo." "Yeyote mwenye kufanya jema uzito wa mdudu chungu mdogo atayaona malipo yake Akhera." "Na yeyote mwenye kufanya baya uzito wa punje ndogo atayaona malipo yake Akhera." {Suratuz zalzala: 1-8]
Tafsiri:
1- "Itakapotikiswa ardhi mtikiso wa nguvu.": Yaani: Itakapotikiswa Ardhi mtikiso mkali utakaotokea siku ya kiyama
2- "Na ikatoa vilivyomo ndani yake: kama wafu" Na Ardhi ikatoa vilivyo ndani ya tumbo lake miongoni mwa wafu na wengineo.
3- "Na akauliza binadamu, kwa babaiko, «Imezukiwa na nini?» Na mwanadamu atasema katika hali ya kubabaika: Ardhi imekuwaje mbona inatikisika na inagonganagongana?!
4- "Siku ya Kiyama ardhi itatoa habari ya mambo iliyofanyiwa ya uzuri na ubaya." Katika siku hiyo kubwa Ardhi itaeleza yale yaliyofanywa juu yake miongoni mwa mazuri na ya shari.
5- "kwa kuwa Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na kutukuka, Ameiamuru itoe habari ya mambo iliyofanyiwa." Kwakuwa Mwenyezi Mungu imefahamisha na akaiamrisha kufanya hivyo.
"Siku hiyo wataondoka kutoka kwenye kisimamo cha Hesabu wakiwa makundi, ili Mwenyezi Mungu Awaonyeshe waliyoyatenda, mazuri na mabaya, na Awalipe kwayo." Katika siku hiyo kubwa ambayo Ardhi itatetemeka ndani yake, watatoka watu kutoka katika kisimamo makundi; Ili wakashuhudie matendo yao waliyoyafanya duniani.
"Yeyote mwenye kufanya jema uzito wa mdudu chungu mdogo atayaona malipo yake Akhera." Atakayefanya kwa uzito wa sisimizi jambo dogo katika matendo ya kheri na wema; ataliona mbele yake.
"Na yeyote mwenye kufanya baya uzito wa punje ndogo atayaona malipo yake Akhera." Na atakayefanya kiasi hicho hicho katika matendo ya shari; basi atakiona mbele yake.