Jawabu: Suratun Nas na tafsiri yake:
Naanza kusoma Qur’an kwa jina la Mwenyezi Mungu nikiomba msaada Wake. «Allah» ni jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa baraka Mwenye kutukuka, Anayestahiki kuabudiwa na sio mwingine. Nalo ni jina mahsusi zaidi miongoni mwa majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, na haitwi kwa jina hili yeyote isipokuwa Yeye Aliyetakasika na sifa za upungufu. «Al-Raḥmān» Mwenye rehema nyingi Ambaye rehema Zake zimewanea viumbe vyote. «Al-Raḥīm» mwenye kuwarehemu Waumini. Na majina mawili haya, kati ya majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, yanakusanya uthibitishaji wa sifa ya urehemefu kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kama unavyonasibiana na haiba Yake.
"Sema, ewe Mtume, «Ninajilinda na kutaka hifadhi kwa Bwana wa watu" "Mfalme wa watu" (2) "Mola wa watu" «Kutokana na udhia wa shetani ambaye hutia watu wasiwasi wanapoghafilika na hujificha atajwapo Mwenyezi Mungu." «Mwenye kupenyeza shari na shaka kwenye vifua vya watu." «Miongoni mwa mashetani wa kijini na kibinadamu.» [Suratun Nas: 1-6]
Tafsiri:
Sema «Najilinda kwa mola wa watu". Sema ewe Mtume- Najikabidhi kwa Mola muumba wa asubuhi, na ninajiweka karibu kwake.
"Mfalme wa watu": Anafanya maamuzi yoyote kwao kwa ayatakayo, hawana mmiliki mwingine zaidi yake.
"Mola wa watu": Muabudiwa wao wa haki, hawana muabudiwa wa kweli mwingine zaidi zake.
«Kutokana na udhia wa shetani ambaye hutia watu wasiwasi wanapoghafilika na hujificha atajwapo Mwenyezi Mungu." Kutokana na shari za shetani ambaye anatia wasi wasi wake kwa watu.
«Mwenye kupenyeza shari na shaka kwenye vifua vya watu." Anapenyeza kwa wasi wasi wake katika nyoyo za watu.
«Miongoni mwa mashetani wa kijini na kibinadamu.» Yaani: Mwenye kutia wasi wasi anakuwa katika binadamu na anakuwa katika majini.