Swali: 15- Soma Suratul Ikhlaswi na uitafsiri.

Jawabu: Suratul Ikhlaswi na tafsiri yake:

Naanza kusoma Qur’an kwa jina la Mwenyezi Mungu nikiomba msaada Wake. «Allah» ni jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa baraka Mwenye kutukuka, Anayestahiki kuabudiwa na sio mwingine. Nalo ni jina mahsusi zaidi miongoni mwa majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, na haitwi kwa jina hili yeyote isipokuwa Yeye Aliyetakasika na sifa za upungufu. «Al-Raḥmān» Mwenye rehema nyingi Ambaye rehema Zake zimewanea viumbe vyote. «Al-Raḥīm» mwenye kuwarehemu Waumini. Na majina mawili haya, kati ya majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, yanakusanya uthibitishaji wa sifa ya urehemefu kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kama unavyonasibiana na haiba Yake.

"Sema, ewe Mtume, «Yeye Ndiye Mwenyezi Mungu Aliyepwekeka kwa ustahiki wa kuabudiwa, uumbaji na utakatifu wa Majina na Sifa, Asiye na mshirika katika hayo." "Mwenyezi Mungu ndiye mkusudiwa" (2) «Hakuzaa wala hakuzaliwa" «Wala hakuna yeyote katika viumbe vyake mwenye kufanana wala kushabihiyananaye katika majina yake, sifa zake wala vitendo vyake.» [Suratul Ikhlaswi: 1-4]

Tafsiri:

"Sema, ewe Mtume, «Yeye ndiye Mwenyezi Mungu aliyepwekeka kwa ustahiki wa kuabudiwa, uumbaji na utakatifu wa Majina na Sifa, Asiye na mshirika katika hayo.": Sema ewe Mtume- Yeye ndiye Mwenyezi Mungu hakuna mungu zaidi yake.

"Mwenyezi Mungu tu ndiye mkusudiwa": Yaani: Hupelekwa kwake shida zote za viumbe.

"Hakuzaa na wala hakuzaliwa": Hana mtoto Mwenyezi Mungu aliyetakasika na kutukuka na wala hana mzazi.

"Na wala hakuna yeyote anayefanananaye hata mmoja": Na wala hajawahi kuwa na mfano wake katika viumbe wake.