Swali: 14- Soma Suratul Masad na uitafsiri.

Jawabu: Suratul Masad na tafsiri yake:

Naanza kusoma Qur’an kwa jina la Mwenyezi Mungu nikiomba msaada Wake. «Allah» ni jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa baraka Mwenye kutukuka, Anayestahiki kuabudiwa na sio mwingine. Nalo ni jina mahsusi zaidi miongoni mwa majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, na haitwi kwa jina hili yeyote isipokuwa Yeye Aliyetakasika na sifa za upungufu. «Al-Raḥmān» Mwenye rehema nyingi Ambaye rehema Zake zimewanea viumbe vyote. «Al-Raḥīm» mwenye kuwarehemu Waumini. Na majina mawili haya, kati ya majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, yanakusanya uthibitishaji wa sifa ya urehemefu kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kama unavyonasibiana na haiba Yake.

"Imepata hasara mikono miwili ya Abu Lahab, na yeye mwenyewe ameangamia" "Haikumfaa mali yake wala alichokichuma" "Ataingia kwenye Moto wenye muwako mkali," "Yeye na mke wake ambaye alikuwa akibeba miba na kuiweka kwenye njia anayopita Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, ili kumuudhi." "Kwenye shingo yake patakuwa na kamba imara iliyosokotwa; atabebewa nayo kwenye Moto wa Jahanamu, kisha atarushwa nayo mpaka chini." [Suratul Masad: 1-5.]

Tafsiri:

"Imepata hasara mikono miwili ya Abu Lahab, na yeye mwenyewe ameangamia" Imepata asara mikono ya baba yake mdogo na Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake, Abuu Lahab bin Abdil Muttwalib kwa hasara aliyoipata ammi yake, kwani alikuwa akimuudhi Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake, na zimebatilika juhudi zake.

"Haikumfaa mali yake wala alichokichuma": Ni kitu gani zimemsaidia mali zake na watoto wake? Hazijamkinga na adhabu, wala hazijamletea rehema.

"Ataingia kwenye Moto wenye muwako mkali," Atauingia siku ya kiyama moto wenye muwako, akichomwa kwa joto lake.

"Yeye na mke wake ambaye alikuwa akibeba miba na kuiweka kwenye njia anayopita Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, ili kumuudhi." Na atauingia mkewe mama Jamil aliyekuwa akimuudhi Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake, kwa kumtupia miba katika njia yake.

"Kwenye shingo yake patakuwa na kamba imara iliyosokotwa; atabebewa nayo kwenye Moto wa Jahanamu, kisha atarushwa nayo mpaka chini.": Shingoni mwake kuna kamba nzito iliyokazwa atakuwa akikokotwa nayo kwenda motoni.