Swali: 13- Soma Suratun Nasri na uitafsiri.

Jawabu: Suratun Nasri na tafsiri yake:

Naanza kusoma Qur’an kwa jina la Mwenyezi Mungu nikiomba msaada Wake. «Allah» ni jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa baraka Mwenye kutukuka, Anayestahiki kuabudiwa na sio mwingine. Nalo ni jina mahsusi zaidi miongoni mwa majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, na haitwi kwa jina hili yeyote isipokuwa Yeye Aliyetakasika na sifa za upungufu. «Al-Raḥmān» Mwenye rehema nyingi Ambaye rehema Zake zimewanea viumbe vyote. «Al-Raḥīm» mwenye kuwarehemu Waumini. Na majina mawili haya, kati ya majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, yanakusanya uthibitishaji wa sifa ya urehemefu kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kama unavyonasibiana na haiba Yake.

"Utakapotimia kwako ewe Mtume, ushindi juu ya makafiri wa Kikureshi na ukaufungua mji wa Makkah." "Na ukaona watu wengi wanaingia kwenye Dini ya Mwenyezi Mungu makundi kwa makundi." "Yatakapotokea hayo, jitayarishe kukutana na Mola Wako kwa kumtakasa, kumhimidi na kumuomba msamaha kwa wingi. Kwani Yeye ni Mwingi wa kuwakubalia toba wenye kumsabihi na kumuomba msamaha, kwa kuwasamehe na kuwarehemu." [Suratun Nasri: 1-3]

Tafsiri:

"Utakapotimia kwako ewe Mtume, ushindi juu ya makafiri wa Kikureshi na ukaufungua mji wa Makkah." Utakapokuja msaada wa Mwenyezi Mungu kwa dini yako ewe Mtume- na utukufu wake, na ukatokea ufunguzi wa Mji wa Makka.

"Na ukaona watu wengi wanaingia kwenye Dini ya Mwenyezi Mungu makundi kwa makundi." Na ukawaona watu wakiingia katika dini ya Mwenyezi Mungu makundi kwa makundi.

"Yatakapotokea hayo, jitayarishe kukutana na Mola Wako kwa kumtakasa, kumhimidi na kumuomba msamaha kwa wingi. Kwani Yeye ni Mwingi wa kuwakubalia toba wenye kumsabihi na kumuomba msamaha, kwa kuwasamehe na kuwarehemu." Basi tambua kuwa hiyo ni alama ya kukaribia kumalizika kwa muda wa kutumwa kwako, basi mtakase mola wako kwa kumshukuru juu ya neema ya ushindi, na kutake kwake msamaha, hakika yeye ni mwingi wa kukubali toba za waja wake, na kuwasamehe.