Jawabu: Suratul Kaafiruun na tafsiri yake:
Naanza kusoma Qur’an kwa jina la Mwenyezi Mungu nikiomba msaada Wake. «Allah» ni jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa baraka Mwenye kutukuka, Anayestahiki kuabudiwa na sio mwingine. Nalo ni jina mahsusi zaidi miongoni mwa majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, na haitwi kwa jina hili yeyote isipokuwa Yeye Aliyetakasika na sifa za upungufu. «Al-Raḥmān» Mwenye rehema nyingi Ambaye rehema Zake zimewanea viumbe vyote. «Al-Raḥīm» mwenye kuwarehemu Waumini. Na majina mawili haya, kati ya majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, yanakusanya uthibitishaji wa sifa ya urehemefu kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kama unavyonasibiana na haiba Yake.
"Sema, ewe Mtume, kuwaambia waliokufuru Mwenyezi Mungu na Mtume wake: «Enyi wenye kumkanusha Mwenyezi Mungu!" «Mimi siabudu mnavyoviabudu miongoni mwa masanamu na waungu wa uongo." «Wala nyinyi si wenye kumuabudu ninayemuabudu.» «Wala mimi si mwenye kuabudu mnavyoviabudu miongoni mwa masanamu na waungu wa uongo." «Wala nyinyi si wenye kuabudu mbeleni ninayemuabudu.» «Nyinyi mna dini yenu mnayoiamini na mimi nina Dini yangu ambayo sitaki nyingine.» [Suratul Kaafiruun: 1-6]
Tafsiri:
«Sema, Enyi wenye kumkanusha Mwenyezi Mungu!" Sema, ewe Mtume, kuwaambia waliomkufuru Mwenyezi Mungu na Mtume wake
«Mimi siabudu mnavyoviabudu miongoni mwa masanamu na waungu wa uongo." Siabudu kwa wakati huu wala wakati ujao mnavyoviabudu miongoni mwa masanamu.
«Wala nyinyi si wenye kumuabudu ninayemuabudu.» Wala nyinyi hamuabudu ninayemuabudu mimi, naye ni Allah peke yake.
«Wala mimi si mwenye kuabudu mnavyoviabudu miongoni mwa masanamu na waungu wa uongo." Wala mimi siabudu mnavyoviabudu miongoni mwa masanamu.
«Wala nyinyi si wenye kuabudu mbeleni ninayemuabudu.» Wala nyinyi hamuabudu ninayemuabudu mimi, naye ni Allah peke yake.
«Nyinyi mna dini yenu mnayoiamini na mimi nina Dini yangu ambayo sitaki nyingine.» Nyinyi mna dini yenu mliyoizusha nyinyi wenyewe, na mimi nina dini yangu aliyoiteremsha Mwenyezi Mungu juu yangu.