Swali: 11- Soma Suratul Kauthar na uitafsiri.

Jawabu: Suratul Kauthar na tafsiri yake:

Naanza kusoma Qur’an kwa jina la Mwenyezi Mungu nikiomba msaada Wake. «Allah» ni jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa baraka Mwenye kutukuka, Anayestahiki kuabudiwa na sio mwingine. Nalo ni jina mahsusi zaidi miongoni mwa majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, na haitwi kwa jina hili yeyote isipokuwa Yeye Aliyetakasika na sifa za upungufu. «Al-Raḥmān» Mwenye rehema nyingi Ambaye rehema Zake zimewanea viumbe vyote. «Al-Raḥīm» mwenye kuwarehemu Waumini. Na majina mawili haya, kati ya majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, yanakusanya uthibitishaji wa sifa ya urehemefu kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kama unavyonasibiana na haiba Yake.

"Hakika sisi tumekupa, ewe Nabii, kheri nyingi za dunia na Akhera." "Basi, swali na uchinje kwa ajili ya mola wako pekee". "Hakika mwenye kukuchukia wewe na kuyachukia uliyokuja nayo ya uongofu na nuru ndiye aliyekatiwa kila kheri." [Suratul Kauthar: 1-3]

Tafsiri:

"Hakika sisi tumekupa, ewe Nabii, kheri nyingi za dunia na Akhera, miongoni mwazo ni mto wa Kauthar ulioko Peponi ambao pambizo zake ni mahema ya lulu na mchanga wake ni miski." Hakika sisi tumekupa ewe Mtume kheri nyingi, na miongoni mwake ni mto wa kauthar ulioko peponi.

"Basi,swali na uchinje wako kwa ajili ya mola wako

, Peke Yake, pamoja na kutaja jina Lake" Tekeleza shukrani kwa Mwenyezi Mungu kwa neema hii, usali kwa ajili yake peke yeke na uchinje kwa ajili yake, kinyume na vile wanavyofanya washirikina kwa kujikurubisha katika masanamu yao kwa kuyachinjia.

"Hakika mwenye kukuchukia wewe na kuyachukia uliyokuja nayo ya uongofu na nuru ndiye itakayekatika athari yake na yeye mwenyewe kukatiwa kila kheri." Hakika mwenye kukuchukia ndiye aliyekatikiwa na kila kheri, aliyesahaulika ambaye akitajwa anatajwa kwa ubaya.