Jawabu: Suratul Maaun na tafsiri yake:
Naanza kusoma Qur’an kwa jina la Mwenyezi Mungu nikiomba msaada Wake. «Allah» ni jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa baraka Mwenye kutukuka, Anayestahiki kuabudiwa na sio mwingine. Nalo ni jina mahsusi zaidi miongoni mwa majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, na haitwi kwa jina hili yeyote isipokuwa Yeye Aliyetakasika na sifa za upungufu. «Al-Raḥmān» Mwenye rehema nyingi Ambaye rehema Zake zimewanea viumbe vyote. «Al-Raḥīm» mwenye kuwarehemu Waumini. Na majina mawili haya, kati ya majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, yanakusanya uthibitishaji wa sifa ya urehemefu kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kama unavyonasibiana na haiba Yake.
"Je, waiona hali ya yule ambaye akanusha kufufuliwa na kulipwa?" "Huyo ndiye yule anayemkaripia yatima kwa nguvu akimnyima haki yake kwa sababu ya ususuavu wa moyo wake." "Na wala hawahimizi wengine kulisha masikini. Vipi yeye mwenyewe atamlisha?." "Adhabu kali itawathibitikia wenye kusali" (4) "ambao wameghafilika na Swala zao: hawazisimamishi kama ipasavyo wala hawazisali kwa nyakati zake." "Ambao huonyesha watu amali zao za kheri kwa njia ya ria." "Na wanazuia misaada" [Suratul Maauun: 1-7]
Tafsiri:
"Je, waiona hali ya yule ambaye akanusha kufufuliwa na kulipwa?" Je umemfahamu anayekanusha kuwepo malipo na siku ya kiyama?
"Huyo ndiye yule anayemkaripia yatima kwa nguvu akimnyima haki yake kwa sababu ya ususuavu wa moyo wake." Huyo ni yule anayemsukuma yatima kwa ukali anapokuwa na haja.
"Na wala hawahimizi wengine kulisha masikini. Vipi yeye mwenyewe atamlisha?." Na wala haihimizi nafsi yake, wala hamuhimizi mwingine juu ya kulisha masikini.
"Adhabu kali itawathibitikia wenye kusali" (4) Maangamivu na adhabu kwa wenye kuswali.
"ambao wameghafilika na Swala zao: hawazisimamishi kama ipasavyo wala hawazisali kwa nyakati zake." Ambao huzipuuza swala zao, hawazijali mpaka wakati wake unapomalizika.
"Ambao huonyesha watu amali zao za kheri kwa njia ya ria." Ambao hujionyesha kwa swala zao na matendo yao, hawatakasi matendo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.
"Na wanazuia misaada": Na wanazuia kuwasaidia wengine kwa vitu ambavyo haviwadhuru endapo watawasaidia.