Swali: 1- Soma Suratul Fatiha na uitafsiri.

Jawabu: Suratul Fatiha na tafsiri yake:

Bismillahir Rahmanir Rahiim (1)" kwa jina la mwenyezi mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu "Alhamdulillaahi Rabbil 'aalamiin" Shukurani zote njema anastahiki mola wa viumbe vyote. "Arrahmaanir rahiim" Mwingi wa Rehema na mwenye kurehemu "Maaliki yaumid-diin" mfalme wa siku ya malipo. "Iyyaakana'budu wa iyyaakanastaiin" wewe tu ndiye tunayekuabudu na wewe tu ndiye tunayekuomba msaada . "Ihdinas swiraatwal mustaqiim" Tuongoze njia iliyonyooka. "Swiraatwalladhiina an 'amta a'laihim, ghairil magh dhuubi a'laihim waladh-dhwaalliin" Njia ya wale uliowaneemesha juu yao, na siyo ya wale uliowakasirikia wala ya wale waliopotea. [Suratul- Faatiha 1-7]

Tafsiri:

Imeitwa kuwa ni suratul faatiha (Kifunguzi); kwa sababu ya kukifungua kitabu cha Mwenyezi Mungu kwa sura hiyo.

{Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu} Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Yaani: Naanza kisomo cha Qur'ani, kwa kutaka msaada kwake Mtukufu nikitaka baraka kwa kutaja jina lake.

{Allah}. Yaani: Muabudiwa kwa haki, na haitwi mwingine jina hilo zaidi yake Mtukufu.

{Al- rahmaan}: Yaani: Mwenye huruma ya hali ya juu, na yenye kuwaenea viumbe wake wote.

{Al rahiim} Mwenye kurehemu: Yaani: Mwenye kuwahurumia waumini.

2- {Kila sifa njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu Mola wa walimwengu}. Yaani: Aina zote za sifa na ukamilifu ni vya Mwenyezi Mungu peke yake.

3- {Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu} Yaani: Mwenye huruma pana ambazo zimekienea kila kitu, na mwenye huruma endelevu kwa waumini.

4- {Mmiliki wa siku ya malipo} Yaani: Ni siku ya kiyama.

5- {Wewe tu tunakuabudu na wewe tu tunakuomba msaada} Yaani: Tunakuabudu wewe peke yako, na tunakuomba msaada wewe peke yako.

6- {Tuongoze njia iliyonyooka} Nao ni uongofu wa kuongoka katika uislamu na mafundisho ya Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake.

7- {Njia ya wale uliowaneemesha juu yao, sio ya wale waliokasirikiwa wala ya wale waliopotea} Yaani: Njia ya waja wema wa Mwenyezi Mungu miongoni mwa Manabii na waliowafuata, na si njia ya wakristo wala Mayahudi.

Na ni sunna mtu aseme baada ya kumaliza kuisoma: (aamin) Yaani: Tukubalie.