Swali: 4- Unatawadha vipi?

Jawabu: Utaosha viganja vya mikono mara tatu.

Na utasukutua na kupandisha maji puani na kuyapenga mara tatu.

Na kusukutua: Ni kuweka maji mdomoni na kuyazungusha na kuyatema.

Na kupandisha maji: Ni kuvuta maji kwa pumzi kuyapandisha ndani ya pua kwa mkono wa kulia.

Na kuyapenga: Nako ni kuyatoa maji puani baada ya kuyapandisha upande wa kushoto.

Kisha kuosha uso mara tatu.

Kisha Kuosha mikono miwili pamoja na viwiko viwili mara tatu.

Kisha kufuta kichwa utaanza mbele ya kichwa kisha utarudisha mikono yako nyuma, na utafuta masikio mawili.

Kisha utaosha miguu yako miwili mpaka katika kongo mbili mara tatu.

Huu ndio ukamilifu, na limethibiti hilo kutoka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake katika hadithi nyingi zilizoko katika Bukhari na Muslim, kazipokea kutoka kwake Othman na Abdallah bin Zaidi na wengineo, Na imethibiti pia kutoka kwake katika kitabu cha Bukhari na wengineo: "Ya kwamba yeye kuna wakati alitawadha mara moja moja, na wakati mwingine alitawadha mara mbili mbili" Yaani: Nikuwa alikuwa akiosha kila kiungo katika viungo vya udhu mara moja, au mara mbili.