Swali: 29- Ni ipi hukumu ya swala ya ijumaa?

Jawabu: Ni faradhi ya lazima kwa kila muislamu mwanaume aliyebalehe mwenye akili na mkazi.

Amesema Allah Mtukufu: "Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mkazifuata Sheria Zake kivitendo! Pindi mwadhini atakapoita kwa ajili ya Swala Siku ya Ijumaa, nendeni upesi msikilize hutuba na mtekeleze Swala, na muache uuzaji na pia ununuaji na kila kinachowashughulisha nyinyi na hiyo Swala. Hilo mliloamrishwa ni bora kwenu nyinyi kutokana na yaliyo humo ya kusamehewa dhambi zenu na kupatiwa malipo mema kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Basi iwapo nyinyi mnayajua manufaa ya nafsi zenu, fanyeni hilo". Kwenye aya hii kuna dalili kwamba kwenda kuhudhuria Swala ya Ijumaa na kusikiliza hutuba ni lazima. [Suratul Munafiquun: 9]