Jawabu: Namna ya kuswali:
1- Anaelekee kibla kwa mwili wake wote, bila kupinda wala kugeuka geuka.
2- Kisha ananuia swala anayotaka kuiswali, anafanya hivyo moyoni mwake bila kuitamka nia.
3- Kisha atatoa takbira ya kuhirimia swala atasema: (Allahu Akbaru), na atanyanyua mikono yake mpaka usawa wa mabega yake wakati wa kutoa takbira.
4- Kisha ataweka kiganja cha mkono wake wa kulia juu ya mgongo wa kiganja cha mkono wake wa kushoto, juu ya kifua chake.
5- Kisha atafungua swala na atasema: "Allaahuma baaid bainiy wabaina khatwaayaaya (Ewe Mwenyezi Mungu weka mbali kati yangu na kati ya makosa yangu) kamaa baa'atta bainal mashriqi wal maghribi (kama ulivyoweka mbali kati ya mashariki na magharibi, Allaahu naqqiniy min khatwaayaaya (Ewe Mwenyezi Mungu nisafishe kutokana na makosa yangu) kamaa yunaqqath-thaubul abyadh minaddanasi (kama inavyosafishwa nguo nyeupe kutokana na uchafu) Allaahummaghsilniy min khatwaayaaya bith-thalji wal maai wal baradi (Ewe Mwenyezi Mungu nioshe mimi kutokana na madhambi kwa barafu na maji na baridi".
"(Sub-hanakallahumma wabihamdika,wa tabaarakasmuka ,wa taalajadduka walaa ilaha ghairuka) -kutakasika ni kwako ewe mola na kushukuriwa ni kwako,limetukuka jina lako,na umetukuka utukufu wako na hakuna mola mwingine zaidi yako-"
6- Kisha ataomba kinga kutokana na shari za shetani, na atasema: "A'udhubillaahi minash-shaitwanir rajiim" Yaani: Ninajikinga kwa Allah kutokana na shetani aliye laaniwa. 7- Kisha atasoma bismillahi na atasoma suratul fatiha, na atasema: Bismillahir Rahmanir Rahiim (1) "Alhamdulillaahi Rabbil 'aalamiin" Shukurani zote njema anastahiki mola wa viumbe vyote (2). "Arrahmaanir rahiim" Mwingi wa Rehema na mwenye kurehemu (3) "Maaliki yaumid-diin" Mmiliki wa Siku ya Malipo (4) "Iyyaaka na'budu wa iyyaaka nasta'iin" Wewe tu ndiye tunayekuabudu na wewe tu ndiye tunayekuomba msaada (5) . "Ihdinas swiraatwal mustaqiim" Tuongoze katika njia iliyonyooka (6). "Swiraatwalladhiina an 'amta a'laihim, ghairil magh dhuubi a'laihim waladh-dhwaalliin" Njia ya wale uliowaneemesha juu yao, na siyo ya wale uliowakasirikia wala ya wale waliopotea (7). [Suratul- Faatiha 1-7]
Kisha anasema: (aaamiin) Yaani: Ewe Mola pokea maombi.
8- Kisha atasoma kiasi anachokiweza katika Qur'ani, na atarefusha kisomo katika swala ya alfajiri.
9- Kisha atarukuu, Yaani: atainamisha mgongo wake kwa kumnyenyekea Mwenyezi Mungu, na atatoa takbira wakati wa kurukuu, na atanyanyua mikono yake mpaka usawa wa mabega yake mawili. Na sunna: anatakiwa anyooshe mgongo wake, na kichwa chake kiwe sawa sawa na mgongo, na ataweka mikono yake juu ya magoti yake mawili akiwa kaachanisha vidole vyake.
10- Na atasema katika rukuu yake: "Sub-haana rabbiyal a'dhwiim" Ametakasika Mola wangu Mtukufu, mara tatu, na kama akiongeza: "Sub-haanaka llaahumma wabihamdika, Allaahummaghfirlii" basi itakuwa vizuri.
11- Kisha atanyanyua kichwa chake kutoka katika rukuu akisema: "Sami'allaahu liman hamidah", na wakati huo akinyanyua mikono yake mpaka usawa wa mabega yake. Na maamuma (anayesalishwa) hatosema: "Sami'allaahu liman hamidah" bali badala yake atasema: "Rabbanaa walakal hamdu" ewe mola wetu sifa njema zote ni zako.
12- Kisha atasema baada ya kunyanyuka kwake: "Rabbanaa walakal hamdu, mil assamaawaati wal ardhwi, wamil amaa shi ita min shai in ba'd"
13- Kisha atasujudu sijida ya kwanza, na atasema wakati wa kusujudu kwake: "Allahu Akbaru", na atasujudu katika viungo vyake saba: Paji la uso na pua, viganja viwili vya mikono, na magoti mawili, na ncha za vidole vya miguu miwili, na atatenganisha kwapa za mikono yake na mbavu zake, na asitandaze mikono yake katika ardhi, na ncha za vidole vyake atazielekeza kibla.
14- Na atasema katika Sijida yake: "Sub-haana rabbiyal a'alaa" Ametakasika Mola wangu aliye juu, mara tatu, na kama akiongeza: "Sub-haanaka llaahumma wabihamdika, Allaahummaghfirlii" basi itakuwa vizuri.
15- kisha atanyanyua kichwa chake kutoka katika sijda huku akisema:"Allahu akbaru".
16- Kisha atakaa kati ya sijda mbili ataukalia mguu wake wa kushoto, na atasimamisha kisigino chake cha kulia, na ataweka mkono wake wa kulia mwisho wa paja lake la kulia karibu na goti, na atakunja vidole viwili, kidole kidogo, na kinachofuata, na atanyanyua kidole cha shahada na atakitikisa wakati wa kuomba kwake dua, na ataweka ncha ya kidole gumba kikiwa sambamba na kidole cha kati kama kimduara hivi, na ataweka mkono wake wa kushoto mwisho wa paja lake la kushoto karibu na goti na vidole vikiwa vimekunjuliwa kuelekea kibla.
17- Na atasema wakati wa kukaa kwake kati ya sijida mbili. "Rabbighfirliiy warahmniiy wahdiniiy warzuquniiy waafiniiy"(Ewe mola wangu nisamehe mimi na unihurumie na uniongoze na uniruzuku na unisamehe)
18- Kisha atasujudu sijida ya pili kama ya kwanza katika yale yanayosemwa na kufanywa, na atatoa takbira wakati wa kusujudu kwake.
19- Kisha atanyanyuka kutoka katika sijida ya pili huku akisema: "Allaahu Akbaru" na ataswali rakaa ya pili kama ya kwanza katika yale yanayosemwa na yanayofanywa, isipokuwa katika rakaa hiyo hatoanza kwa dua ya ufunguzi.
20- Kisha atakaa baada ya kumaliza rakaa ya pili huku akisema: "Allaahu Akbaru", na atakaa kama anavyokaa kati ya sijida mbili hivyo hivyo.
21- Na atasoma tahiyatu katika kikao hiki, na atasema: "Attahiyyaatulillahi,Waswalawaatu watwayyibaatu,Assalaamu Alaika Ayyuha Nabiyyu Wrahmatullahi Wabarakaatuhu, Assalaamu Alaina waalaa ibadillahi swaalihiina, Ash-hadu an-laailaha illa llau wa anna muhamadan rasuulullahi"Allahumma swalli alaa muhammad waalaa ali muhammad, kamaa swalaita alaa ibrahiim waalaa aali ibrahiim Innaka hamiidun majiid,Allahumma Baariki Alaa Muhammad wa alaa aali muhammad ,kamaa baarakta alaa ibraahiim wa- alaa aali ibrahiim innaka hamiidun majiid" Au'dhubillahi min adhabi Jahannam, wami adhabil kabri, wamin fitinatil mahyaa wal mamaati, wamin fitinatila masihid dajjali" Kisha atamuomba mola wake kwa yale anayoyataka katika kheri za dunia na akhera.
22- Kisha atatoa salamu kuliani kwake atasema: "Assalaamu alaikum warahmatullaah" Na kushotoni kwake hivyo hivyo.
23- Na ikiwa ni swala ni ya rakaa tatu au nne; atasimama wakati wa kumalizika kwa tahiyatu ya kwanza, nayo ni: "Ash-hadu an laa ilaaha illa llaahu, wa ash-hadu anna Muhammadan abduhu warasuuluhu".
24- Kisha atasimama wima huku akisema: "Allahu Akbaru", na atanyanyua mikono yake usawa wa mabega yake wakati huo.
25- Kisha atasali kumazia kiasi kilichobakia katika swala yake kwa namna kama ilivyokuwa rakaa ya tatu, isipokuwa hapa ataishia katika kusoma suratul fatiha.
26- Kisha atakaa (tawaruku) yaani: atakalia kalio la kushoto na kusimamisha mguu wa kulia, na atautoa nje mguu wa kushoto kupitia katika muundi wa mguu wa kulia, na ataweka makalio yake katika ardhi, na ataweka mikono yake juu ya mapaja yake kama alivyoiweka katika tahiyatu ya kwanza.
27- Na atasoma katika kikao hiki tahiyatu yote.
28- Kisha atatoa salamu kuliani kwake atasema: "Assalaamu alaikum warahmatullaah" Na kushotoni kwake hivyo hivyo.