Jawabu: Ni sunna kumi na moja, kama zifuatazo:
1- Ni kauli ya mswaliji baada ya takbira ya kuhirimia swala: "Sub-haanakallaahumma wabihamdika, watabaaraka smuka, wata'ala jadduka, walaa ilaaha ghairuka" Na hii huitwa dua ya ufunguzi wa swala.
2- kuomba kinga kutokana na shetani aliyelaaniwa.
3- Bismillah.
4- Kauli ya: Aamin.
5- kusoma sura nyingine baada ya suratul Faatiha.
6- Kudhihirisha kisomo kwa imamu.
7- Kauli ya kusema baada ya neno la rukuu (Rabbanaa walakal hamdu) kusema; Mil assamaawaati, wamil al Ardhwi, wamila maa shiita, min shai in ba'd"
8- Kila kinachozidi katika tasbihi ya rukuu: Yaani: kumsabihi Mwenyezi Mungu kwa mara ya pili na ya tatu, na zaidi ya hapo.
9- Kinachozidi zaidi ya mara moja katika tasbihi ya sijida.
10- Kinachozidi zaidi ya mara moja katika kauli kati ya sijida mbili: "Rabbighfirlii".
11- Kuwataki rehema familia ya Mtume Amani iwe juu yao katika tashahudi ya mwisho, na kumuombea baraka yeye na wao, na kuomba dua ya hapo.
Ya nne: Sunna za vitendo, na huitwa mikao (mionekano):
1- kunyanyua mikono pamoja na takbira ya kuhirimia swala.
2- Na wakati wa kurukuu.
3- Na wakati wa kunyanyuka kutoka katika rukuu.
4- Na kuiachia baada ya hapo.
5- Kuweka mkono wa kulia juu ya kushoto.
6- Kutazama mahali pa kusujudia.
7- Kuachanisha kati ya miguu miwili wakati wa kusimama.
8- Kushika magoti mawili kwa mikono miwili vidole vikiwa vimeachanishwa katika rukuu, na kunyoosha mgongo hapo, na kukifanya kichwa kilingane na mgongo.
9- Kuhakikisha viungo vya kusujudu viko katika ardhi, na viguse mahala pa kusujudia.
10- Kutenganisha kati ya mikono na mbavu, na tumbo lake na mapaja yake, na mapaja yake na miundi yake, na kuiachanisha na magoti, na kusimamisha visigino viwili, na kuweka tumbo za vidole vya miguu miwili katika ardhi vikiwa vimeachanishwa, na mtu aweke mikono yake usawa wa mabega yake ikiwa imekunjuliwa na vidole vikiwa vimefungamanishwa.
11- Kukaa mkao wa kukalia mguu wa kushoto na kusimamisha wa kulia (Iftirashi) katika kikao kati ya sijida mbili, na katika tahiyatu ya kwanza, na kukalia kalio la kushoto na kulaza mguu wa kushoto ndani ya mguu wa kulia (Tawaruku) katika tahiyatu ya pili.
12- Kuweka mikono miwili juu ya mapaja mawili ikiwa imetandazwa, vidole vikiwa vimebananishwa kati ya sijida mbili, na hivyo hivyo katika tahiyatu, isipokuwa katika tahiyatu ataukunja mkono wa kulia kidole kidogo na kinachofuata, na atafanya duara kati ya kidole cha kati na kidole gumba, na ataashiria kwa kidole cha shahada wakati wa kumtaja Mwenyezi Mungu.
13- Mtu kugeuka kulia na kushoto wakati wa kutoa salamu.