Swali: 21- Ni ngapi idadi ya nguzo za swala?

Jawabu: Ni nguzo kumi na nne, kama ifuatavyo:

Ya kwanza: Kusimama katika swala za faradhi kwa mwenye kuweza.

Takbira ya kuhirimia swala, nayo ni kusema "Allaahu Akbaru" wakati wa kuanza swala.

Kusoma Suratul Fatiha.

Kurukuu, na atanyoosha mgongo wake uwe sawa sawa na ataweka kichwa chake kiwe sambamba.

Kunyanyuka kutoka katika rukuuu.

Kusimama wima.

Kusujudu, na kuhakikisha paji la uso wake liko chini, na pua yake, na viganja vyake, na magoti yake, na ncha ya vidole vya miguu yake kuwa mahali anaposujudia.

Kunyanyuka kutoka katika sijida.

Kukaa kati ya sijida mbili.

Na sunna: Ni akae akiwa kaukalia mguu wake wa kushoto na kaunyoosha wa kulia, na auelekeze kibla.

Utulivu, nako ni kutulia katika kila nguzo ya kivitendo.

Tashahudi ya mwisho.

Kukaa kwa ajili ya tashahudi.

Salamu mbili, nako ni mtu kusema mara mbili: "Assalaamu alaikum warahmatullaah".

Kupangilia nguzo -kama tulivyosema-, ikiwa atasujudu kwa mfano kabla ya kurukuu kwa makusudi; swala itabatilika, na kwa kusahau; itamlazimu arudi ili arukuu, kisha asujudu.