Swali: 8-Ni ipi maana ya Ibada?

Jawabu: Ni jina linalokusanya yale yote anayoyapenda Mwenyezi Mungu na kuyaridhia katika maneno na matendo ya siri na ya wazi.

Matendo ya wazi: Mfano kama kumtaja Mwenyezi Mungu kwa ulimi, miongoni mwa tasbihi (kusema Sub-haanallaah) na tahmidi (kusema Alhamdulillaah) na takbiri (kusema Allaahu Akbar) na swala na Hijja.

Matendo ya siri: Mfano kama kumtegemea Mwenyezi Mungu na kuwa na hofu na matumaini.