Swali: 6- Nini Maana ya kushuhudia kuwa Muhammad ni mtume wa Mwenyezi Mungu?

Jawabu: Maana yake: Ni kuwa Mwenyezi Mungu kamtuma kwa walimwengu wote ili awape habari njema na awaonye.

Na ni wajibu:

1- Kumtii katika yale aliyoyaamrisha.

2- Kumsadikisha katika yale aliyoyaeleza.

3- Kutomuasi.

4- Asiabudiwe Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa yale aliyoyafundisha kama sheria, nako ni kuiga kupitia mafundisho yake (Sunna) na kuacha uzushi.

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Mwenye kumtii Mtume basi hakika atakuwa kamtii Mwenyezi Mungu" [Suratun Nisaa: 80], na akasema Mtukufu "Na hatamki kwa matamanio 3- Bali huo ni ufunuo anafunuliwa" [Surat Najm: 3,4]. Na anasema aliyetakasika na kutukuka: {Hakika nyinyi mna kiigizo chema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa anaye mtaraji Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na akamkumbuka Mwenyezi Mungu na kumtaja kwa wingi} ((21)), [Suratul Israi: 21].