Jawabu: Kuamrisha mema: Ni kuamrisha katika kila ambalo ni la kumtii Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka, na uovu: Ni kukataza kila maasi ya kumuasi Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka.
Amesema Allah Mtukufu: "Nyinyi, enyi umma wa Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, ni umma bora na ni watu wenye manufaa zaidi kwa watu, mnaamrisha mema, nayo ni yale yanayofahamika uzuri wake kisheria na kiakili, na mnakataza maovu , nayo ni yale yanayoeleweka ubaya wake kisheria na kiakili, na mnamuamini Mwenyezi Mungu kikweli-kweli imani inayotiliwa nguvu na vitendo." [Surat Al Imran: 110]