Jawabu: Neno la Tauhidi ni "Laa ilaaha illa llaahu" Na maana yake: Ni kuwa hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu pekee.
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Basi tambua ya kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu" [Suratu Muhammad: 19]