Jawabu: Imani inaongezeka kwa kumtii Mwenyezi Mungu na inapungua kwa kufanya maasi.
Amesema Allah Mtukufu: "Hakika wenye kumuamini Mwenyezi Mungu ni wale ambao akitajwa Mwenyezi Mungu hulainika nyoyo zao na wasomewapo aya za Mwenyezi Mungu zinawazidishia Imani na kwa Mola wao wanategemea" [surat Anfaal:2]