Swali: 35- Ni akina nani vipenzi wa Mwenyezi Mungu Mtukufu? (Mawalii).
Jawabu: Ni waumini wachamungu.
Amesema Allah Mtukufu: "Tambueni kuwa vipenzi wa Mwenyezi Mungu hawatokuwa na hofu juu yao na wala hawatohuzunika, (62) Wale walioamini na wakawa wachamungu" [Suratu Yunus: 62,63].