Swali: 34- Ni upi wajibu wetu mbele ya wanachuoni wa waislamu?

Jawabu: Tunatakiwa kuwapenda na kurejea kwao katika maswala mbali mbali na yale yanayotokea katika mambo ya sheria, na hatuwasemi ila kwa mazuri, na mwenye kuwataja kwa mambo tofauti na hayo katika mambo mabaya; basi huyu atakuwa hayuko katika njia sahihi.

Amesema Allah Mtukufu: "Mwenyezi Mungu Anawapandisha vyeo wale Waumini miongoni mwenu, na Anawapandisha vyeo wale wenye elimu daraja nyingi kwa kuwapatia malipo mema na daraja za kupata radhi. Na Mwenyezi Mungu Anayatambua matendo yenu, hakuna chochote kinachofichikana Kwake katika hayo, na Yeye ni mwenye kuwalipa nyinyi kwayo" {Suratul Mujadila: 11].