Jawabu: Allah: maana yake ni Mola muabudiwa wa kweli, yeye pekee asiye na mshirika wake.
Arrabbu (Bwana): Yaani: Muumba na mmiliki mgawa riziki na mpangiliaji yeye peke yake aliyetukuka.
Assamiiu: Ambaye usikivu wake umekienea kila kitu, na anazisikia sauti zote pamoja na kutofautiana kwake na kuwa na aina mbali mbali.
Albaswiru: Anaye kiona kila kitu, na anakiona kila kitu kiwe kidogo au kikubwa.
Al A'liimu: Naye ni yule ambaye elimu yake imekizunguka kila kitu kilichopita na kilichopo na kijacho.
Alrahman: Ambaye huruma yake imekienea kila kiumbe na kila kilicho hai, waja wote na viumbe vyote viko chini ya huruma yake.
Arrazzaaq: Ambaye anajukumu la kugawa riziki kwa viumbe wote kuanzia watu na majini na wanyama wote.
Al hayyu: Aliye hai ambaye hafi, na viumbe wote wanakufa.
Al A'dhwiim: Mwenye ukamilifu wote na utukufu wote katika majina yake na sifa zake na vitendo vyake.