Jawabu: Hofu: Ni kumuogopa Mwenyezi Mungu na kuogopa adhabu zake.
Kutaraji: Ni kutaraji thawabu za Mwenyezi Mungu na msamaha wake na rehema zake.
Na ushahidi ni kauli yake Allah Mtukufu: "Hao washirikina wanawaomba, miongoni mwa Manabii, watu wema na Malaika, wao wenyewe wanashindana kujiweka karibu na Mola wao kwa matendo mema wanayoyaweza, wanatarajia rehema Yake na wanaogopa adhabu Yake. Hakika adhabu ya Mola wako ndiyo ambayo inatakikana kwa waja wawe na tahadhari nayo na waiogope(adhabu ya moto)". [Suratul Israai: 57]. Na amesema Allah Mtukufu: {Wape habari, ewe Mtume, waja wangu kwamba mimi ni mwenye kuwasamehe Waumini wenye kutubia, ni mwenye huruma kwao 49 Na kwamba adhabu yangu ndiyo adhabu iumizayo}. [Suratul Hijri: 49,50].