Swali: Ni nani Mtume wa mwisho na manabii?

Jawabu: Ni Muhammad Rehema na Amani ziwe juu yake.

Amesema Allah Mtukufu: {Muhammad si baba wa yeyote katika wanaume wenu, bali ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na Mwisho wa Manabii} [Suratul Ahzaab: 40]. -Na Amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu rehema na Amani ziwe juu yake. "Na mimi ndiye mwisho wa Manabii hakuna Nabii baada yangu" Imepokelewa na Abuu Daud na Tirmidhiy na wengineo.