Jawabu:
1- Unafiki mkubwa: Nao ni kuficha ukafiri na kudhihirisha imani.
Na huu unamtoa mtu katika uislamu nao ni katika ukafiri mkubwa.
Amesema Allah Mtukufu: "Hakika wanafiki watakuwa katika tabaka la chini kabisa motoni na wala hawatompata yeyote wa kuwanusuru" [Suratun Nisaa: 145]
2- Unafiki mdogo:
Kuongopa na kutotimiza ahadi na kufanya hiyana katika amana.
Na huu haumtoi mtu katika uislamu, nao ni katika madhambi na mfanyaji anajitia katika adhabu.
Amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu rehema na Amani ziwe juu yake. "Alama za Mnafiki ni tatu: Anapozungumza husema uongo, na anapoahidi huenda kinyume, na akiaminiwa hufanya hiyana". Ameipokea Bukhari na Muslim.