Swali: 2- Ni ipi dini yako?

Jawabu: Dini yangu ni uislamu: Nao Ni kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu kwa kumpwekesha, na kunyenyekea kwa kumtii, na kujiepusha na ushirikina pamoja na washirikina.

Amesema Allah Mtukufu: "Hakika dini inayo kubaliwa kwa Mwenyezi Mungu ni Uislamu" [Surat Al Imran: 19]