Swali: 19- Taja itikadi ya kupendana kwa ajili ya Allah na kutengana kwa ajili yake.

Jawabu: Kupendana: Ni mapenzi ya waumini na kusaidizana kwao.

Amesema Allah Mtukufu: {Na Waumini wanaume na Waumini wanawake wao kwa wao ni marafiki}. [Suratu Tauba: 71].

Na kutengana kwa ajili ya Allah: Ni kuwachukia makafiri na kuwafanyia uadui.

Amesema Allah Mtukufu: "Hakika imekuwa kwenu nyinyi ni kiigizo chema kwa Ibrahim na wale waliopamoja naye, pale waliposema kuwaambia watu wao; 'Hakika sisi tumejitenga mbali na yale mnayoyaabudu kinyume na Mwenyezi Mungu, tumekupingeni na umedhihiri kati yetu sisi na nyinyi uadui na chuki milele mpaka mumuamini Mwenyezi Mungu peke yake" [Suratul Mumtahina: 4]