Jawabu: Ni kila walichokizua watu katika dini, na wala hakikuwepo katika zama za Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake na maswahaba zake.
*Hapana, hatuukubali na tunaukataa.
Kwa kauli yake Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake: "Kila uzushi ni upotovu" Imepokelewa na Abuu Daud
Na mfano wake: Ni kuongeza katika ibada, kama kuzidisha katika udhu kuosha mara ya nne, na kama kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume, haya hayakupokelewa kutoka kwa Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake na maswahaba zake.