Swali: 16- Ni nini maana ya Qur'ani?

Jawabu: Ni maneno ya Mwenyezi Mungu mtukufu, hayajaumbwa.

Amesema Allah Mtukufu: "Na pindi yeyote, miongoni mwa washirikina, akiomba kuingia kwenye himaya yako, ewe Mtume, na akataka amani, basi mkubalie maombi yake ili apate kuyasikia maneno ya Mwenyezi Mungu mtukufu na auone uongofu wake," [Suratu Tauba: 6].