Jawabu: Kumuamini Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Ni kumuamini Mwenyezi Mungu kuwa yeye ndiye aliyekuumba na akakuruzuku, na yeye ndiye Mfalme na mpangiliaji peke yake wa viumbe vyote.
Naye ndiye muabudiwa, hakuna muabudiwa kwa haki zaidi yake.
Na kuwa yeye ni Mtukufu Mkuu aliye kamilika Mwenye sifa zote, na ana majina mazuri mno na sifa za hali ya juu, hana mshirika, na hakimfanani chochote Mtukufu.
Kuamini Malaika:
Nao ni viumbe kawaumba Mwenyezi Mungu kwa Nuru, na kwa ajili ya kumuabudu yeye na kwa ajili ya utiifu mkamilifu katika amri zake.
-Miongoni mwao ni Jibrili Amani iwe juu yake anayeteremka na ufunuo (Wahyi) kwa Manabii.
Kuamini vitabu:
Navyo ni vitabu alivyo viteremsha Allah juu Mitume wake.
Kama Qur'ani: Kwa Muhammad Rehema na Amani ziwe juu yake.
-Injili: kwa Issa- Amani iwe juu yake.
-Taurati: kwa Mussa- Amani iwe juu yake.
-Zaburi: kwa Daudi- Amani iwe juu yake.
-Nyaraka za Ibrahim Amani iwe juu yao: Ibrahim na Mussa.
Kuamini mitume:
Nao ni wale aliowatuma Mwenyezi Mungu kwa waja wake ili wawafundishe, na wawabashirie mazuri na pepo, na wawaonye dhidi ya shari na moto.
-Na wabora wao ni wenye uthubutu, (ulul a'zmi) Nao ni:
Nuhu Amani iwe juu yake.
Ibrahim Amani iwe juu yake.
Mussa Amani iwe juu yake.
Issa Amani iwe juu yake.
Muhammad Rehema na Amani ziwe juu yake.
Kuamini siku ya mwisho:
Nayo ni yale yatakayo kuwa baada ya kifo katika makaburi, na siku ya kiyama, na siku ya kufufuliwa na kuhesabiwa, kiasi ambacho watatulizana watu wa peponi katika makazi yao, na watu motoni katika makazi yao.
Kuamini Makadirio kheri yake na shari yake.
Makadirio: Ni kuitakidi kuwa Mwenyezi Mungu anajua kila kitu kinachotokea katika ulimwengu, na kuwa yeye alikiandika katika ubao uliohifadhiwa, na akataka kutokea kwake na kukiumba kwake.
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hakika sisi kila kitu tumekiumba kwa makadirio". [Suratul Qamar: 49].
Nayo yako katika daraja nne:
Daraja ya kwanza: Ni Elimu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na miongoni mwake ni elimu yake iliyokitangulia kila kitu, kabla ya kutokea kwa vitu na baada ya kutokea kwake.
Na ushahidi wake ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hakika Mwenyezi Mungu, Peke Yake, Anajua ni lini Kiyama kitasimama. Na Yeye Ndiye Anayeteremsha mvua kutoka mawinguni, hakuna awezaye hilo yeyote isipokuwa Yeye. Na Anajua vilivyomo ndani ya vizazi vya wanawake. Na Anajua kitakachotendwa na kila mtu wakati ujao. Na hakuna nafsi inayojua itafia wapi. Ni Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Peke Yake Ndiye Anayehusika kwa kujua hayo yote. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mtambuzi, Ameyazunguka mambo ya nje na ya ndani, hakuna chochote katika hayo kinachofichikana Kwake." [Suratu Luqman: 34].
Daraja ya pili: Nikuwa Mwenyezi Mungu aliandika hilo katika ubao uliohifadhiwa, kila kitu kilichotokea na kitakachotokea basi kimeandikwa kwake katika kitabu.
Na ushahidi wake ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na ziko kwake funguo za ghaibu; hakuna azijuaye ila Yeye tu. Na Yeye anajua kilichoko nchi kavu na baharini. Na halidondoki jani ila analijua. Wala punje katika giza la ardhi, wala kinyevu, wala kikavu ila vyote hivyo vimo katika Kitabu kinacho bainisha} (59), [Suratul An'am: 59].
Daraja ya tatu: Nayo ni kuwa kila kitu kinatokea kwa matakwa ya Mwenyezi Mungu na wala hakitokei kitu kwake wala kwa viumbe wake isipokuwa ni kwa matakwa yake Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Na ushahidi wake ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Atakayetaka miongoni mwenu anyooke katika njia. (28) na wala hamuwezi kutaka nyinyi isipokuwa atake Mwenyezi Mungu Mola mlezi wa walimwengu wote (29)" [Suratut takwiri: 28,29]
Daraja ya nne: Ni kuamini kuwa kila kilichopo kimeumbwa, alikiumba Mwenyezi Mungu, na aliumba dhati yake na sifa zake na harakati zake, na kila kitu kinachoambatana nacho.
Na ushahidi wake ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na Mwenyezi Mungu amekuumbeni na hayo mnayoyafanya. (96)" [Suratu Swafat: 96].