Jawabu: 1- Kumuamini Mwenyezi Mungu Mtukufu.
2- Na Malaika wake.
3- Na vitabu vyake.
4- Na Mitume wake.
5- Na siku ya mwisho.
6- Na makadirio kheri yake na shari yake.
Na ushahidi: Ni hadithi ya Jibrili ambayo ni mashuhuri iko katika sahihi Muslim, alisema Jibrili kumwambia Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake. "Basi nieleze kuhusu imani, akasema: Ni kumuamini Mwenyezi Mungu na Malaika wake na vitabu vyake na Mitume wake na siku ya mwisho na kuamini makadirio kheri yake na shari yake."