Swali: 13- Je! kuna yeyote anayejua ghaibu (mambo yaliyofichikana) zaidi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu?

Jawabu: Hakuna ajuaye ghaibu isipokuwa Mwenyezi Mungu pekee,

Alisema Allah Mtukufu: "Sema, ewe Mtume, kuwaambia wao, «Hakuna yeyote ajuaye, mbinguni wala ardhini, jambo lolote lililofichikana ambalo Mwenyezi Mungu Amejihusisha Mwenyewe kulijua. Na wao hawajui ni lini watafufuliwa kutoka makaburini mwao wakati wa Kiyama kusimama.» [Suratun Namli: 65]