Jawabu: Ushirikina: Ni kuielekeza aina yoyote miongoni mwa aina za ibada kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Aina zake:
Shirki kubwa; Mfano: Kumuomba asiyekuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, au kumsujudia asiyekuwa yeye Mtakasifu, au kuchinja kwa ajili ya asiyekuwa Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka.
Shirki ndogo; Mfano: Kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, au mahirizi, nayo ni yale yanayotundikwa kwa ajili ya kuleta manufaa au kuzuia madhara, na shirki ndogo kabisa ni kujionyesha, mfano kama mtu kupendezesha swala yake kwa kuwa anaona kuna watu wanamtazama.