Jawabu: Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu Mtukufu na kitu kingine.
Amesema Allah Mtukufu: "Hakika Mwenyezi Mungu, Hamsamehi aliyemshirikisha Yeye na yeyote miongoni mwa viumbe Wake au akamkufuru kwa aina yoyote ya ukafiri mkubwa. Lakini Anayasamehe na kuyafuta madhambi yaliyo chini ya ushirikina kwa Anayemtaka miongoni mwa waja Wake. Na yeyote anayemshirikisha Mwenyezi Mungu na mwingine, hakika amefanya dhambi kubwa. [Suratun Nisaa: 48]