Jawabu: 1- Tauhidur rubuubiya (Tauhidi ya ulezi) Nayo ni kuamini kuwa Mwenyezi Mungu ndiye muumbaji, mgawa riziki Mmiliki na mpangiliaji, yeye pekee asiye na mshirika wake.
2- Tauhidul uluuhiyya (Tauhidi ya uungu): Nayo ni kumpwekesha Mwenyezi Mungu kwa ibada, asiabudiwe yeyote ila Mwenyezi Mungu Mtukufu.
3- Tauhidul Asmaai wasswifaati (Tauhidi ya majina na sifa): Nayo ni kuyaamini majina na sifa za Mwenyezi Mungu Mtukufu zilizokuja katika kitabu cha Mwenyezi Mungu na mafundisho ya Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-, bila kupiga mfano wala kushabihisha wala kupotosha.
Na ushahidi wa aina hizi tatu za tauhidi: Ni kauli yake Mtukufu: «Yeye Ndiye Mwenyezi Mungu, Mola wa mbingu na ardhi na vilivyomo baina yake, Ndiye Mmiliki, Muumba na Mwendeshaji wa hivyo vyote, basi muabudu Yeye Peke Yake, ewe Nabii, na uvumilie katika kumtii, wewe na waliokufuata, Hana mfano Wake kitu chochote katika dhati Yake, sifa Zake na vitendo Vyake.» [Suratu Mariam: 65].