SEHEMU YA SHERIA.

Jawabu: Twahara: Ni kuondoa uchafu usioonekana, na kuondoka kwa uchafu.

Kusafisha uchafu: Nako ni muislamu kuondoa yaliyodondoka katika najisi katika mwili wake, au juu thawabu zake, na katika eneo au mahalali panaposwaliwa hapo.

Twahara ya hadathi: Nao ni usafi unaokuwa kwa udhu au kuoga, kwa maji masafi, au kutayammamu kwa atakayekosa maji, au akawa na dharura ya kutotumia maji.

Jawabu: Kwa kukiosha kwa maji mpaka kisafishike.

-Na ama alichokilamba mbwa; kitaoshwa mara saba mara moja kwa udongo.

Jawabu: Amesema Mtume Sala na amani ziwe juu yake: "pindi muislamu au muumini atakapo tawadha akaosha uso wake, madhambi yake yote yanayo tokana na kuangalia yanaondoka na tone la maji usoni mwake, akiosha mikono yake yanaondoka madhambi yote yatokanayo na mikono kutokana na tone la mwisho, akiosha miguu yake madhambi yote yatokanayo na kutembea yanaondoka na tone la mwisho, mpaka mwislamu anabaki msafi hana madhambi". Imepokelewa na Imamu Muslim

Jawabu: Utaosha viganja vya mikono mara tatu.

Na utasukutua na kupandisha maji puani na kuyapenga mara tatu.

Na kusukutua: Ni kuweka maji mdomoni na kuyazungusha na kuyatema.

Na kupandisha maji: Ni kuvuta maji kwa pumzi kuyapandisha ndani ya pua kwa mkono wa kulia.

Na kuyapenga: Nako ni kuyatoa maji puani baada ya kuyapandisha upande wa kushoto.

Kisha kuosha uso mara tatu.

Kisha Kuosha mikono miwili pamoja na viwiko viwili mara tatu.

Kisha kufuta kichwa utaanza mbele ya kichwa kisha utarudisha mikono yako nyuma, na utafuta masikio mawili.

Kisha utaosha miguu yako miwili mpaka katika kongo mbili mara tatu.

Huu ndio ukamilifu, na limethibiti hilo kutoka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake katika hadithi nyingi zilizoko katika Bukhari na Muslim, kazipokea kutoka kwake Othman na Abdallah bin Zaidi na wengineo, Na imethibiti pia kutoka kwake katika kitabu cha Bukhari na wengineo: "Ya kwamba yeye kuna wakati alitawadha mara moja moja, na wakati mwingine alitawadha mara mbili mbili" Yaani: Nikuwa alikuwa akiosha kila kiungo katika viungo vya udhu mara moja, au mara mbili.

Jawabu: Ni zile ambazo hausihi au haukamiliki udhu wa muislamu atakapoacha moja kati yake.

1- Kuosha uso ikiwa ni pamoja na kusukutua na kupandisha maji puani.

2- Kuosha mikono miwili mpaka katika viwiko viwili.

3- Kufuta kicha pamoja na masikio mawili.

4- Kuosha miguu miwili mpaka katika kongo mbili.

5- Kupangilia kati ya viungo, aoshe uso, kisha mikono miwili, kisha afute kichwa, kisha aoshe miguu miwili.

6- Kufululiza: Nako ni kushika udhu kwa muda wa kufuatana, bila kutenganisha nyakati mpaka maji yakauke katika viungo.

- Kama mtu kutawadha nusu ya udhu, kisha aache aje kuukamilisha katika wakati mwingine, udhu wake hausihi (haukubaliki)

Jawabu: Sunna za udhu: ni zile ambazo kama mtu atazifanya basi atapata ziada ya malipo na thawabu, na kama akiziacha hana dhambi, na udhu wake utakuwa sahihi.

1- Kusema: Bismillaahi.

2- Kupiga mswaki.

3- Kuosha viganga viwili.

4- Kuachanisha vidole.

5- kuosha kwa mara ya pili na ya tatu katika viungo.

6- Kuanzia kulia.

7- Dua baada ya udhu: "Nina shuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu peke yake hana mshirika, na nina shuhudia kuwa Muhammad ni mja wake na ni mtume wake".

8- Swala ya rakaa mbili baada ya udhu.

Jawabu: Ni kile kinachotoka katika njia mbili, ya mbele na ya nyuma, kama haja ndogo au kubwa au upepo.

Kulala, au wendawazimu au kuzimia.

kula nyama ya Ngamia.

Kugusa utupu wa mbele au wa nyuma bila kizuizi.

Jawabu: Tayammamu ni kutumia udongo au kinginecho katika udongo wa ardhi, wakati wa kukosa maji, au dharura ya kutotumia maji.

Jawabu: Ni kupiga udongo mpigo mmoja kwa viganja viwili, na kufuta uso na juu ya viganja viwili mara moja.

Jawabu: Ni vitenguzi vyote vya udhu.

ziada ya hapo, ni yatakapopatikana maji.

Jawabu: Khofu mbili: Ni viatu vinavyovaliwa mguuni vilivyotokana na ngozi.

Soksi mbili: Ni vitu vinavyo valiwa mguuni ambavyo si vya ngozi.

Ni sheria kufuta juu yake badala ya kuosha miguu miwili.

Jawabu: Ni wepesi na kuondoa uzito kwa waja, hasa hasa nyakati za baridi, na masika na safarini, kiasi ambacho inakuwa tabu kuvua vilivyoko miguuni.

Jawabu: 1- Awe amezivaa akiwa na twahara, yaani baada ya udhu.

2- Khofu ziwe safi (Twahara) haifai kufuta juu ya najisi.

3- Khofu ziwe zinafunika mahala palazima kuoshwa kwake katika udhu.

4- Kufuta kuwe ndani ya muda maalumu uliowekwa, mkazi ambaye si msafiri: afute ndani ya mchana na usiku wake, na kwa msafiri: ni siku tatu usiku na mchana wake (Masaa 72)

Jawabu: Ama namna ya kufuta ni: aweke vidole vya mikono yake vikiwa vimeloa maji juu ya vidole vya miguu yake kisha anavitembeza mpaka katika muundi wake, atafuta mguu wa kulia kwa mkono wa kulia, na mguu wa kushoto kwa mkono wa kushoto, na ataachanisha vidole vyake na wala asirudie kupitisha, yaani afanye mara moja.

Jawabu: 1- Kumalizika kwa muda wa kufuta, haitakiwi kufuta juu ya khofu baada ya kumalizika kikomo cha muda wa kufuta kisheria, mchana na usiku wake kwa mwenyeji, na michana mitatu na usiku wake kwa msafiri.

2- Kuvua khofu mbili, akivua mtu khofu mbili au moja wapo baada yakuwa amefuta, kufuta juu yake kutakuwa kumebatilika.

Jawabu: Swala: Ni kumuabudu Mwenyezi Mungu kwa kauli na matendo maalumu, yanayoanza kwa takbiri (Allahu Akbaru) yanayohitimishwa kwa salamu.

Jawabu: Swala ni lazima kwa kila muislamu

Amesema Allah Mtukufu: "Hakika swala kwa waumini ni faradhi iliyowekewa muda maalumu". [Surat Nisaa: 103]

Jawabu: Kuacha swala ni ukafiri, Amesema Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake: "Ahadi iliyopo kati yetu na wasiokuwa waislamu ni swala, na atakayeiacha swala basi atakuwa kakufuru" Ameipokea Ahmad na Tirmidhiy na wengineo.

Jawabu: Ni swala tano mchana na usiku, Swala ya Alfajiri: Rakaa mbili, Na swala ya Adhuhuri: Rakaa nne, Na swala ya Lasiri: Rakaa nne, Na swala ya maghribi: Rakaa tatu, na swala ya Ishaa: Rakaa nne.

Jawabu: 1- Uislamu; haitosihi kwa kafiri.

2- Akili; haikubaliki kwa mwendawazimu.

3- Kupambanua; haikubaliki kwa mtoto mdogo ambaye hajafikia umri wa kupambanua mambo.

4- Nia.

5- kuingia wakati wa swala.

6- Twahara kwa ajili ya kuondoa uchafu (Hadathi).

7- Kujisafisha kutokana na najisi.

8- Kusitiri uchi.

9- Kuelekea kibla.

Jawabu: Ni nguzo kumi na nne, kama ifuatavyo:

Ya kwanza: Kusimama katika swala za faradhi kwa mwenye kuweza.

Takbira ya kuhirimia swala, nayo ni kusema "Allaahu Akbaru" wakati wa kuanza swala.

Kusoma Suratul Fatiha.

Kurukuu, na atanyoosha mgongo wake uwe sawa sawa na ataweka kichwa chake kiwe sambamba.

Kunyanyuka kutoka katika rukuuu.

Kusimama wima.

Kusujudu, na kuhakikisha paji la uso wake liko chini, na pua yake, na viganja vyake, na magoti yake, na ncha ya vidole vya miguu yake kuwa mahali anaposujudia.

Kunyanyuka kutoka katika sijida.

Kukaa kati ya sijida mbili.

Na sunna: Ni akae akiwa kaukalia mguu wake wa kushoto na kaunyoosha wa kulia, na auelekeze kibla.

Utulivu, nako ni kutulia katika kila nguzo ya kivitendo.

Tashahudi ya mwisho.

Kukaa kwa ajili ya tashahudi.

Salamu mbili, nako ni mtu kusema mara mbili: "Assalaamu alaikum warahmatullaah".

Kupangilia nguzo -kama tulivyosema-, ikiwa atasujudu kwa mfano kabla ya kurukuu kwa makusudi; swala itabatilika, na kwa kusahau; itamlazimu arudi ili arukuu, kisha asujudu.

Jawabu: Wajibu za swala, nazo ni nane, kama ifuatavyo:

1- Takbira zote isipokuwa takbira ya kuhirimia swala (Ile kuanza swala)

2- Kauli ya: "Samiallaahu liman hamidah" kwa imamu na anayeswali peke yake.

3- Kauli ya: Rabbanaa walakal hamdu".

4- kauli ya: "Sub-haana rabbiyal A'dhwiim" mara moja katika rukuu.

5- kauli ya: "Sub-haana rabbiyal A'laa" mara moja katika sijida.

6- kauli ya: "Rabbighfirli" kati ya sijida mbili.

7- Tahiyatu ya kwanza.

8- kukaa kwa ajili ya tahiyatu ya kwanza.

Jawabu: Ni sunna kumi na moja, kama zifuatazo:

1- Ni kauli ya mswaliji baada ya takbira ya kuhirimia swala: "Sub-haanakallaahumma wabihamdika, watabaaraka smuka, wata'ala jadduka, walaa ilaaha ghairuka" Na hii huitwa dua ya ufunguzi wa swala.

2- kuomba kinga kutokana na shetani aliyelaaniwa.

3- Bismillah.

4- Kauli ya: Aamin.

5- kusoma sura nyingine baada ya suratul Faatiha.

6- Kudhihirisha kisomo kwa imamu.

7- Kauli ya kusema baada ya neno la rukuu (Rabbanaa walakal hamdu) kusema; Mil assamaawaati, wamil al Ardhwi, wamila maa shiita, min shai in ba'd"

8- Kila kinachozidi katika tasbihi ya rukuu: Yaani: kumsabihi Mwenyezi Mungu kwa mara ya pili na ya tatu, na zaidi ya hapo.

9- Kinachozidi zaidi ya mara moja katika tasbihi ya sijida.

10- Kinachozidi zaidi ya mara moja katika kauli kati ya sijida mbili: "Rabbighfirlii".

11- Kuwataki rehema familia ya Mtume Amani iwe juu yao katika tashahudi ya mwisho, na kumuombea baraka yeye na wao, na kuomba dua ya hapo.

Ya nne: Sunna za vitendo, na huitwa mikao (mionekano):

1- kunyanyua mikono pamoja na takbira ya kuhirimia swala.

2- Na wakati wa kurukuu.

3- Na wakati wa kunyanyuka kutoka katika rukuu.

4- Na kuiachia baada ya hapo.

5- Kuweka mkono wa kulia juu ya kushoto.

6- Kutazama mahali pa kusujudia.

7- Kuachanisha kati ya miguu miwili wakati wa kusimama.

8- Kushika magoti mawili kwa mikono miwili vidole vikiwa vimeachanishwa katika rukuu, na kunyoosha mgongo hapo, na kukifanya kichwa kilingane na mgongo.

9- Kuhakikisha viungo vya kusujudu viko katika ardhi, na viguse mahala pa kusujudia.

10- Kutenganisha kati ya mikono na mbavu, na tumbo lake na mapaja yake, na mapaja yake na miundi yake, na kuiachanisha na magoti, na kusimamisha visigino viwili, na kuweka tumbo za vidole vya miguu miwili katika ardhi vikiwa vimeachanishwa, na mtu aweke mikono yake usawa wa mabega yake ikiwa imekunjuliwa na vidole vikiwa vimefungamanishwa.

11- Kukaa mkao wa kukalia mguu wa kushoto na kusimamisha wa kulia (Iftirashi) katika kikao kati ya sijida mbili, na katika tahiyatu ya kwanza, na kukalia kalio la kushoto na kulaza mguu wa kushoto ndani ya mguu wa kulia (Tawaruku) katika tahiyatu ya pili.

12- Kuweka mikono miwili juu ya mapaja mawili ikiwa imetandazwa, vidole vikiwa vimebananishwa kati ya sijida mbili, na hivyo hivyo katika tahiyatu, isipokuwa katika tahiyatu ataukunja mkono wa kulia kidole kidogo na kinachofuata, na atafanya duara kati ya kidole cha kati na kidole gumba, na ataashiria kwa kidole cha shahada wakati wa kumtaja Mwenyezi Mungu.

13- Mtu kugeuka kulia na kushoto wakati wa kutoa salamu.

Jawabu: (1) Kuacha nguzo au sharti katika sharti za swala.

(2) Kuzungumza kwa makusudi.

(3) Kula au kunywa.

(4) Harakati nyingi za kufululiza.

(5) Kuacha wajibu miongoni mwa wajibu za swala kwa makusudi.

Jawabu: Namna ya kuswali:

1- Anaelekee kibla kwa mwili wake wote, bila kupinda wala kugeuka geuka.

2- Kisha ananuia swala anayotaka kuiswali, anafanya hivyo moyoni mwake bila kuitamka nia.

3- Kisha atatoa takbira ya kuhirimia swala atasema: (Allahu Akbaru), na atanyanyua mikono yake mpaka usawa wa mabega yake wakati wa kutoa takbira.

4- Kisha ataweka kiganja cha mkono wake wa kulia juu ya mgongo wa kiganja cha mkono wake wa kushoto, juu ya kifua chake.

5- Kisha atafungua swala na atasema: "Allaahuma baaid bainiy wabaina khatwaayaaya (Ewe Mwenyezi Mungu weka mbali kati yangu na kati ya makosa yangu) kamaa baa'atta bainal mashriqi wal maghribi (kama ulivyoweka mbali kati ya mashariki na magharibi, Allaahu naqqiniy min khatwaayaaya (Ewe Mwenyezi Mungu nisafishe kutokana na makosa yangu) kamaa yunaqqath-thaubul abyadh minaddanasi (kama inavyosafishwa nguo nyeupe kutokana na uchafu) Allaahummaghsilniy min khatwaayaaya bith-thalji wal maai wal baradi (Ewe Mwenyezi Mungu nioshe mimi kutokana na madhambi kwa barafu na maji na baridi".

"(Sub-hanakallahumma wabihamdika,wa tabaarakasmuka ,wa taalajadduka walaa ilaha ghairuka) -kutakasika ni kwako ewe mola na kushukuriwa ni kwako,limetukuka jina lako,na umetukuka utukufu wako na hakuna mola mwingine zaidi yako-"

6- Kisha ataomba kinga kutokana na shari za shetani, na atasema: "A'udhubillaahi minash-shaitwanir rajiim" Yaani: Ninajikinga kwa Allah kutokana na shetani aliye laaniwa. 7- Kisha atasoma bismillahi na atasoma suratul fatiha, na atasema: Bismillahir Rahmanir Rahiim (1) "Alhamdulillaahi Rabbil 'aalamiin" Shukurani zote njema anastahiki mola wa viumbe vyote (2). "Arrahmaanir rahiim" Mwingi wa Rehema na mwenye kurehemu (3) "Maaliki yaumid-diin" Mmiliki wa Siku ya Malipo (4) "Iyyaaka na'budu wa iyyaaka nasta'iin" Wewe tu ndiye tunayekuabudu na wewe tu ndiye tunayekuomba msaada (5) . "Ihdinas swiraatwal mustaqiim" Tuongoze katika njia iliyonyooka (6). "Swiraatwalladhiina an 'amta a'laihim, ghairil magh dhuubi a'laihim waladh-dhwaalliin" Njia ya wale uliowaneemesha juu yao, na siyo ya wale uliowakasirikia wala ya wale waliopotea (7). [Suratul- Faatiha 1-7]

Kisha anasema: (aaamiin) Yaani: Ewe Mola pokea maombi.

8- Kisha atasoma kiasi anachokiweza katika Qur'ani, na atarefusha kisomo katika swala ya alfajiri.

9- Kisha atarukuu, Yaani: atainamisha mgongo wake kwa kumnyenyekea Mwenyezi Mungu, na atatoa takbira wakati wa kurukuu, na atanyanyua mikono yake mpaka usawa wa mabega yake mawili. Na sunna: anatakiwa anyooshe mgongo wake, na kichwa chake kiwe sawa sawa na mgongo, na ataweka mikono yake juu ya magoti yake mawili akiwa kaachanisha vidole vyake.

10- Na atasema katika rukuu yake: "Sub-haana rabbiyal a'dhwiim" Ametakasika Mola wangu Mtukufu, mara tatu, na kama akiongeza: "Sub-haanaka llaahumma wabihamdika, Allaahummaghfirlii" basi itakuwa vizuri.

11- Kisha atanyanyua kichwa chake kutoka katika rukuu akisema: "Sami'allaahu liman hamidah", na wakati huo akinyanyua mikono yake mpaka usawa wa mabega yake. Na maamuma (anayesalishwa) hatosema: "Sami'allaahu liman hamidah" bali badala yake atasema: "Rabbanaa walakal hamdu" ewe mola wetu sifa njema zote ni zako.

12- Kisha atasema baada ya kunyanyuka kwake: "Rabbanaa walakal hamdu, mil assamaawaati wal ardhwi, wamil amaa shi ita min shai in ba'd"

13- Kisha atasujudu sijida ya kwanza, na atasema wakati wa kusujudu kwake: "Allahu Akbaru", na atasujudu katika viungo vyake saba: Paji la uso na pua, viganja viwili vya mikono, na magoti mawili, na ncha za vidole vya miguu miwili, na atatenganisha kwapa za mikono yake na mbavu zake, na asitandaze mikono yake katika ardhi, na ncha za vidole vyake atazielekeza kibla.

14- Na atasema katika Sijida yake: "Sub-haana rabbiyal a'alaa" Ametakasika Mola wangu aliye juu, mara tatu, na kama akiongeza: "Sub-haanaka llaahumma wabihamdika, Allaahummaghfirlii" basi itakuwa vizuri.

15- kisha atanyanyua kichwa chake kutoka katika sijda huku akisema:"Allahu akbaru".

16- Kisha atakaa kati ya sijda mbili ataukalia mguu wake wa kushoto, na atasimamisha kisigino chake cha kulia, na ataweka mkono wake wa kulia mwisho wa paja lake la kulia karibu na goti, na atakunja vidole viwili, kidole kidogo, na kinachofuata, na atanyanyua kidole cha shahada na atakitikisa wakati wa kuomba kwake dua, na ataweka ncha ya kidole gumba kikiwa sambamba na kidole cha kati kama kimduara hivi, na ataweka mkono wake wa kushoto mwisho wa paja lake la kushoto karibu na goti na vidole vikiwa vimekunjuliwa kuelekea kibla.

17- Na atasema wakati wa kukaa kwake kati ya sijida mbili. "Rabbighfirliiy warahmniiy wahdiniiy warzuquniiy waafiniiy"(Ewe mola wangu nisamehe mimi na unihurumie na uniongoze na uniruzuku na unisamehe)

18- Kisha atasujudu sijida ya pili kama ya kwanza katika yale yanayosemwa na kufanywa, na atatoa takbira wakati wa kusujudu kwake.

19- Kisha atanyanyuka kutoka katika sijida ya pili huku akisema: "Allaahu Akbaru" na ataswali rakaa ya pili kama ya kwanza katika yale yanayosemwa na yanayofanywa, isipokuwa katika rakaa hiyo hatoanza kwa dua ya ufunguzi.

20- Kisha atakaa baada ya kumaliza rakaa ya pili huku akisema: "Allaahu Akbaru", na atakaa kama anavyokaa kati ya sijida mbili hivyo hivyo.

21- Na atasoma tahiyatu katika kikao hiki, na atasema: "Attahiyyaatulillahi,Waswalawaatu watwayyibaatu,Assalaamu Alaika Ayyuha Nabiyyu Wrahmatullahi Wabarakaatuhu, Assalaamu Alaina waalaa ibadillahi swaalihiina, Ash-hadu an-laailaha illa llau wa anna muhamadan rasuulullahi"Allahumma swalli alaa muhammad waalaa ali muhammad, kamaa swalaita alaa ibrahiim waalaa aali ibrahiim Innaka hamiidun majiid,Allahumma Baariki Alaa Muhammad wa alaa aali muhammad ,kamaa baarakta alaa ibraahiim wa- alaa aali ibrahiim innaka hamiidun majiid" Au'dhubillahi min adhabi Jahannam, wami adhabil kabri, wamin fitinatil mahyaa wal mamaati, wamin fitinatila masihid dajjali" Kisha atamuomba mola wake kwa yale anayoyataka katika kheri za dunia na akhera.

22- Kisha atatoa salamu kuliani kwake atasema: "Assalaamu alaikum warahmatullaah" Na kushotoni kwake hivyo hivyo.

23- Na ikiwa ni swala ni ya rakaa tatu au nne; atasimama wakati wa kumalizika kwa tahiyatu ya kwanza, nayo ni: "Ash-hadu an laa ilaaha illa llaahu, wa ash-hadu anna Muhammadan abduhu warasuuluhu".

24- Kisha atasimama wima huku akisema: "Allahu Akbaru", na atanyanyua mikono yake usawa wa mabega yake wakati huo.

25- Kisha atasali kumazia kiasi kilichobakia katika swala yake kwa namna kama ilivyokuwa rakaa ya tatu, isipokuwa hapa ataishia katika kusoma suratul fatiha.

26- Kisha atakaa (tawaruku) yaani: atakalia kalio la kushoto na kusimamisha mguu wa kulia, na atautoa nje mguu wa kushoto kupitia katika muundi wa mguu wa kulia, na ataweka makalio yake katika ardhi, na ataweka mikono yake juu ya mapaja yake kama alivyoiweka katika tahiyatu ya kwanza.

27- Na atasoma katika kikao hiki tahiyatu yote.

28- Kisha atatoa salamu kuliani kwake atasema: "Assalaamu alaikum warahmatullaah" Na kushotoni kwake hivyo hivyo.

Jawabu: "Astaghfirullaah" Mara tatu.

"Allahumma antassalaam, waminkassalaam, tabaarakta yaa dhaljalaali wal ikraam".

"Laailaha illa llahu wah'dahu laa shirika lahu ,lahulmulku walahulhamduwhuwa alaa kulli shain qadiir, "Allahuma laa maania limaa aa'twaita walaa muutwiya limaa mana'ata walaa yanfau dhaljaddi minkal jaddu".

"Laa ilaaha illa llaahu wahdahu Laa shariika lahu, Lahul Mulku walahul Hamdu wahuwa a'laa kulli shai in qadiir, Laa haulaa walaa quwwata illaa billaah, walaa na'budu illaa iyyaahu, Lahun ni'matu walahul Fadhlu, walahuth thanaaul hasan, Laa ilaaha Illa llaahu Mukhliswiina lahud diina walau karihal kaafiruun" Yaani: Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, yeye pekee asiye na mshirika, Ufalme ni wake na sifa njema ni zake, naye juu ya kila kitu ni muweza, Hakuna ujanja wala nguvu ila kwa Mwenyezi Mungu, Hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu, Na hakuna tunayemuabudu ila yeye, ana neema na ana fadhila, na ana sifa njema, Hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu tunamtakasia dini hata kama makafiri watachukia.

"Sub-haana llaah" Mara thelathini na tatu.

"Alhamdulillaah" Mara thelathini na tatu.

"Allaahu Akbaru" Mara thelathini na tatu.

kisha atasema kukamilisha mia moja: "Laailaha illa llahu wah'dahu laa sharika lahu ,lahulmulku walahulhamdu wahuwa alaa kulli shain qadiir"

Na atasoma suratul Ikhlaswi (Qul huwallaahu) na sura mbili za kinga (Falaq na Nasi) mara tatu baada ya swala ya alfajiri na magharibi, na mara moja baada ya swala zingine.

Na atasoma ayatul kursiy mara moja

Jawabu: Rakaa mbili kabla ya alfajiri.

Rakaa nne kabla ya Adhuhuri.

Rakaa mbili baada ya adhuhuri.

Rakaa mbili baada ya magharibi.

Rakaa mbili baada ya Ishaa.

Ubora wake: Kasema Mtume Rehema na amani ziwe juu yake: "Atakayeswali mchana na usiku rakaa kumi na mbili za hiyari, basi Mwenyezi Mungu atamjengea nyumba peponi" Kaipokea Muslim na Ahmad na wengineo.

Jawabu: Ni siku ya ijumaa, Amesema Mtume Sala na amani ziwe juu yake: "Hakika katika siku zenu bora ni siku ya ijumaa, ndani yake kaumbwa Adam, na ndani yake alifariki, na ndani yake litapulizwa baragumu na ndani yake utatokea ukelele, basi zidisheni ndani yake kunitakia rehema juu yangu kwani dua zenu za rehema huletwa kwangu". Akasema: Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ni vipi dua zetu zinaletwa kwako na hali tayari uko katika udongo? Akasema: "Hakika Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka ameiharamishia ardhi mili ya Manabii". Imepokelewa na Abudaud na Tirmidhiy na wengineo.

Jawabu: Ni faradhi ya lazima kwa kila muislamu mwanaume aliyebalehe mwenye akili na mkazi.

Amesema Allah Mtukufu: "Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mkazifuata Sheria Zake kivitendo! Pindi mwadhini atakapoita kwa ajili ya Swala Siku ya Ijumaa, nendeni upesi msikilize hutuba na mtekeleze Swala, na muache uuzaji na pia ununuaji na kila kinachowashughulisha nyinyi na hiyo Swala. Hilo mliloamrishwa ni bora kwenu nyinyi kutokana na yaliyo humo ya kusamehewa dhambi zenu na kupatiwa malipo mema kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Basi iwapo nyinyi mnayajua manufaa ya nafsi zenu, fanyeni hilo". Kwenye aya hii kuna dalili kwamba kwenda kuhudhuria Swala ya Ijumaa na kusikiliza hutuba ni lazima. [Suratul Munafiquun: 9]

Jawabu: Idadi ya rakaa za swala ya ijumaa ni mbili, imamu atasoma kwa sauti ndani ya rakaa hizo, kiasi ambacho zitatanguliwa na hotuba mbili zenye kueleweka.

Jawabu: Haitakiwi kuacha kwenda katika swala ya ijumaa isipokuwa kwa udhuru wa kisheria, na imekuja kutoka kwa Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake, kauli yake: "Atakayeacha ijumaa tatu kwa kuzipuuzia; Mwenyezi Mungu hupiga muhuri katika moyo wake" Imepokelewa na Abudaud na Tirmidhiy na wengineo.

Jawabu:

1- Kuoga.

2- Kutumia manukato.

3- Kuvaa nguo nzuri.

4- Kuwahi mapema msikitini.

5- Kukithirisha kumswalia Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake.

6- Kusoma suratul kahf.

7- Kwenda msikitini kwa kutembea kwa miguu.

8- Kuitafuta saa ya kujibiwa maombi.

Jawabu: Kutoka kwa Abdallah bin Omari Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, ya kwamba Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake: "Swala ya pamoja ni bora kuliko swala ya mtu mmoja kwa daraja ishirini na saba". Imepokelewa na Imamu Muslim

Jawabu: Ni moyo kuhudhuria na viungo kutulia ndani yake.

Amesema Allah Mtukufu: "Kwa hakika wamefaulu wenye kumuamini Mwenyezi Mungu". "Wale ambao miongoni mwa sifa zao ni kwamba wao ni wanyenyekevu kwenye Swala zao, nyoyo zinajishughulisha na hiyo Swala tu na viungo vyao vimetulia ." [Suratul Mu'uminun: 1,2]

Jawabu: Ni haki ya wajibu katika mali maalumu katika wakati maalumu.

- Nayo ni nguzo katika nguzo za uislamu, na ni sadaka ya wajibu inachukuliwa kutoka kwa mwenye uwezo na kupewa fakiri.

Amesema Allah Mtukufu: (Na toeni zaka) [Suratul Baqara: 43].

Jawabu: Ni ile isiyokuwa zaka, mfano: kutoa sadaka ya kitu chochote katika njia za kheri katika wakati wowote.

Amesema Allah Mtukufu: "Na toeni katika njia ya Mwenyezi Mungu". [Suratul Baqara: 195].

Jawabu: Ni kumuabudu Mwenyezi Mungu kwa kujizuia kutokana na vyenye kufunguza kwanzia kuchomoza alfajiri mpaka kuzama jua, pamoja na nia, nayo ina aina mbili:

Swaumu ya wajibu: Mfano: kufunga mwezi wa ramadhani, nayo ni nguzo katika nguzo za uislamu.

Amesema Allah Mtukufu: "Enyi mlioamini mmelazimishwa kufunga saumu kama walivyolazimishwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu." [Suratul Baqara: 183].

Na funga isiyokuwa ya wajibu: Mfano kufunga siku ya juma tatu na alhamisi kila wiki, na kufunga siku tatu katika kila mwezi, na bora zaidi ni masiku meupe (Tarehe: 13,14,15) katika kalenda ya mwezi (Hijiria).

Jawabu: Kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, ya kwamba Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake: "Atakayefunga ramadhani kwa imani na kwa kutaraji malipo, atasamehewa madhambi yake yaliyotangulia." Hadithi hii wamekubaliana Bukhari na Muslim.

Jawabu: Kutoka kwa Abuu Saidi Al khudriy Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, Amesema: amesema Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake: "Hakuna mja yeyote atakayefunga siku moja katika njia ya Mwenyezi Mungu, isipokuwa Mwenyezi Mungu atauweka mbali kwa siku hiyo moja uso wake na moto misimu sabini". Hadithi hii wamekubaliana Bukhari na Muslim.

Maana ya "Misimu sabini" Yaani: Miaka sabini.

Jawabu: Kula na kunywa kwa makusudi.

2- Kujitapisha kwa makusudi.

3- Kuritadi kutoka katika uislamu.

Jawabu: 1- Kuwahi kufungua.

2- Daku, pamoja na kuichelewesha kwake.

3- Kuongeza juhudi katika amali za kheri miongoni mwa ibada.

4- Kauli ya mfungaji anapotukanwa: Hakika mimi nimefunga.

5- Kuomba dua wakati wa kufuturu.

6- Kufungua kwa tende mbichi au kavu, ikiwa hatopata; basi hata kwa maji.

Jawabu: Hija: Ni kufanya ibada kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwa kukusudia kwenda katika nyumba yake tukufu kwa ajili ya matendo maalumu na katika wakati maalumu.

Amesema Allah Mtukufu: {Na Mwenyezi Mungu amewawajibishia watu wafanye Hijja katika nyumba hiyo, yule awezaye kufunga safari kwenda huko, na atakayekanusha (Na asiende na haliyakuwa anauwezo) Basi Mwenyezi Mungu si muhitaji wa kuwahitajia walimwengu} [97]. [Surat Al Imr: 97]

Jawabu: 1- Kuhirimia. (kutia nia ya kuanza Hija)

2- Kusimama katika uwanja wa Arafa.

3- Twawafu (Mzunguko katika Alkaaba) wa kumalizia.

4- Kukimbia mchaka mchaka kati ya Swafa na Marwa.

Jawabu: Kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, amesema: Nilimsikia Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake akisema: "Mwenye kuhiji na akawa hakusema maneno machafu wala kutenda matendo machafu, anarudi kama alivyo zaliwa na mama yake (akiwa hana dhambi). Ameipokea Bukhari na wengineo.

(Kama siku aliyozaliwa na mama yake) yaani: hana dhambi.

Jawabu: Umra: Ni kufanya ibada kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwa kukusudia kwenda katika nyumba yake tukufu kwa ajili ya matendo maalumu na katika wakati wowote.

Jawabu: 1- Kuhirimia. (kutia nia ya kuanza Umra)

2- Kutufu katika nyumba (Alkaaba)

3- Kukimbia mchaka mchaka kati ya Swafa na Marwa.

Jawabu: Ni kutoa juhudi na wakati katika kuueneza uislamu na kuutetea na kuwatetea waislamu, au kupigana na adui wa uislamu na waislamu.

Amesema Allah Mtukufu: "Na piganeni jihadi kwa mali zenu na nafsi zenu katika njia ya Mwenyezi Mungu. Haya ni kheri kwenu ikiwa mnajua" [Suratu Tauba: 41].